Na serikali ni nani? Mbona serikali inasema Katiba ni nzuri na watu wapige kura ya Ndiyo?
Tumia kichwa chako kifikiri na siyo kufugia nywele!
Mimi nitaamini Waraka wa Baraza la Maulamaa na sio Bakwata ya ccm
kwa hiyo serikali na maccm wanavyozungumzia mambo ya mahakama ya kadhi kwani yenyewe ni madhehebu ya dini?
Kardinali Pengo alisema hivi;
Hawana nguvu za kumjibu Kardinali Pengo na wanachofanya ni kuzunguka mbuyu na kutafuta easy target!
Wewe ndio tumia akili yako, serikali inaongozwa na mwenyekiti wa CCM. CCM ndio iliyopewa ridhaa ya kuongoza nchi na kuunda serikali. Kwani maaskofu wameteuliwa au kupewa mamlaka yao na chama gani cha siasa?
Kati yao na kardinal pengo nani ana nguvu sasa
Hawa ndio maskofu wenye uzalendo na nchi yao
Kamanda Greenwhich hawa ndio wazalendo tunaowataka kwenye nchi hiiAskofu Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amepinga vikali kauli ya serikali kwamba maaskofu wamegawanyika kuhusu Kura ya Hapana kwenye Katiba Mpya.
Askofu Bagonza ambaye ni mjumbe wa CCT ameonya kauli ya Samwel Sitta kwamba Serikali haitarudi nyuma kuhusu katiba mpya.
Askofu Bagonza ambaye ana msimamo thabiti amesema wapo maaskofu wa mfukoni wanaoandaliwa na Serikali ambao wanatumika kujibu hoja mbalimbali za kanisa.
Akizungumzia Kauli ya Kadinali Pengo kupingana na maaskofu wenzake, Askofu Bagonza amesema huo ni msimamo binafsi wa Kadinali Pengo na siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.
Askofu Bagonza amesema msimamo wa Kanisa Katoliki nchini unatolewa na TEC ambalo ni Baraza la Maaskofu Katoliki nchini.
Askofu Bagonza amesisitiza kwamba pamoja na msimamo binafsi wa Kadinali Pengo lakini ameruhusu Tamko la Maaskofu kusomwa katika Makanisa yote ya Jimbo lake la DSM.
Askofu Bagonza ameishangaa serikali kusema Kanisa halina haki ya kuwataka waumini kupiga kura ya Hapana.
Askofu Bagonza amesema.." Kama CCM na serikali yake wanawashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie,iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?"...alihoji.
======================
Chanzo: Mwananchi
CCM ni chama cha siasa, hayo ya kuwaambia wachague nini kwenye masuala ya siasa ndio jukumu lao. Sasa hao maaskofu ni chma cha siasa?
Pengo ana mamlaka kwa jimbo lake tu na si majimbo mengine. Msemaji wa TEC ni rais wake. Kura ni hapana
Pengo ana mamlaka kwa jimbo lake tu na si majimbo mengine. Msemaji wa TEC ni rais wake. Kura ni hapana
Muislam yeyote angetoa kauli kama hiii, ungeskia mengine saa hii, defender kama 120 na askari FFU kama 70 hivi na wajeda kadhaa mlangoni kwa mtoa kauli, hii ni iwapo tu Muislam 1 angetoa kauli kama ya huyu kiongozi wa kanisa lenye wafuasi wengi zaidi duniani kusema waumini wapige kura ya hapana????