Askofu Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amepinga vikali kauli ya serikali kwamba maaskofu wamegawanyika kuhusu Kura ya Hapana kwenye Katiba Mpya.
Askofu Bagonza ambaye ni mjumbe wa CCT ameonya kauli ya Samwel Sitta kwamba Serikali haitarudi nyuma kuhusu katiba mpya.
Askofu Bagonza ambaye ana msimamo thabiti amesema wapo maaskofu wa mfukoni wanaoandaliwa na Serikali ambao wanatumika kujibu hoja mbalimbali za kanisa.
Akizungumzia Kauli ya Kadinali Pengo kupingana na maaskofu wenzake, Askofu Bagonza amesema huo ni msimamo binafsi wa Kadinali Pengo na siyo msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.
Askofu Bagonza amesema msimamo wa Kanisa Katoliki nchini unatolewa na TEC ambalo ni Baraza la Maaskofu Katoliki nchini.
Askofu Bagonza amesisitiza kwamba pamoja na msimamo binafsi wa Kadinali Pengo lakini ameruhusu Tamko la Maaskofu kusomwa katika Makanisa yote ya Jimbo lake la DSM.
Askofu Bagonza ameishangaa serikali kusema Kanisa halina haki ya kuwataka waumini kupiga kura ya Hapana.
Askofu Bagonza amesema.." Kama CCM na serikali yake wanawashawishi watu wapige kura ya Ndiyo, Ukawa wamewaeleza watu wao wasusie,iweje iwe tatizo kwa Jukwaa la Wakristo kuwaeleza wafuasi wao wapige kura ya Hapana?"...alihoji.
======================
Chanzo: Mwananchi