Kuna wageni wengi Mbezi. Wamama zaidi ya watatu ninao wafahamu wamepata ndoa za ukubwani na Wamarekani weusi.Je! Kuna Jamii au watu especially mataifa ya nje wanaozungumza kingereza??? Kama hakuna huo ni ushamba...
Kwa hiyo watoto wa mbezi beach hawajui kiswahili na wazazi ambao ni watanzania mnaona fahari watoto wenu hawajui kiswahili? 😂😂Sababu ya kutumia lugha ya kingereza kwa watoto ni kwamba asilimia 98 ya watoto wa sunday school mbezi beach wanasoma shule za english medium au international school na walimu wanapata ugumu kuwafundisha kwa kiswahili
Na hata mafunzo ya kipaimara wameweka option ya english na kiswahili, mtoto anachagua anachoweza
Chini ya Mibuyu, lakini nako tupu, lazima uwe na kuku wa kafara!Sasa makabwela watasali Wapi!
Unajua anglican ni church of england. Hii kitu sio mchezo tunabishana tu ila bado tunahitaji ukombozi kifikra. Lugha na utamaduni ni njia imefanikiwa sana kwa sisi waafrika kuendelea kutawaliwa kifikra. Ukitawaliwa kama taifa lazima ubakie maskini.Bwashee sali misa ya kwanza.
Binafsi naona wamechelewa sana kuanzisha hii misa ya kiinglishi.
Kanisani kwetu pale Anglican St Alban Huduma kwa lugha ya malkia ina zaidi ya miaka 100 sasa.........Ni misa ya pili.
Ya kwanza na ya tatu ni za kiswahili!
Sababu ya kutumia lugha ya kingereza kwa watoto ni kwamba asilimia 98 ya watoto wa sunday school mbezi beach wanasoma shule za english medium au international school na walimu wanapata ugumu kuwafundisha kwa kiswahili
Na hata mafunzo ya kipaimara wameweka option ya english na kiswahili, mtoto anachagua anachoweza
Tena wakazie iwe kila week maana ni muhimuIbada ya kingereza kkt mbezi beach ni once a month, na ni option sio unalazimishwa, binafsi mimi na watoto wangu tunasali engkish service na first born wangu mafundisho ameopt english kwa sababu ndio lugha amekua akiitumia shule na tuliona kiswahili kitasumbua
Cha mshingi wewe chagua ibada unayoimudu, kama ni kiswagili au kingereza
Ndio mpango uliopo kwa sasaTena wakazie iwe kila week maana ni muhimu
Nashangaa sana awamu hii mtu anataka upangiwe hadi ibada ya kusali kisa wanataka kukuza kiswahiliKama mtoto anaweza chagua anachotaka mtu mzima kinamshinda nn kuchagua sehemu ya kupata huduma anayotaka.
Waache watu waishi maisha yao wanayopenda as far hawavunji sheria za nchi!
Wanajua kiswahili, binafsi wa kwangu anajua kiswahili lakini kinamsumbua, kumbuka shuleni since grade one anasoma masomo yote kwa.lugha ya kingereza, anapofika grade 3 ndio anaanza kusoma somo moja la kiswahili, unadhani hapo ni lugha gani atakua ameimaster sana kati ya english na kiswahili? Dunia imebadilika na maisha yamebadilika, ni lazima wazazi pia tujifunze kuadapt ulimwengu uliopo la sivyo watoto wetu watabaki nyumaKwa hiyo watoto wa mbezi beach hawajui kiswahili na wazazi ambao ni watanzania mnaona fahari watoto wenu hawajui kiswahili? [emoji23][emoji23]
Kuna misa ya kiswahili na kiingereza. Muumini unachagua inayokufaa. Na tukumbuke kuwa Tanzania hatuishi watanzania peke yetu, tuna wageni ambao wangependelea zaidi misa ya Kiingereza.
Na kwa vile makanisa yako mengi, mtu akiona anakwazika kwa sababu muda walioamua kuwa na misa ya kiingereza ndio muda ambao angependa kusali basi anaweza kuhamia kanisa lingine la dhehebu hilo hilo ambalo halina misa za kiingereza.
Naamini viongozi wa kanisa hili wameona kuna waumini ambao wangependa kuabudu kwa lugha hiyo. Nao kama wachungaji wa Bwana hawawezi kuachia kondoo wao wapotee kwa kitu ambacho ambacho kiko ndani ya uwezo wao.
Amandla...
Ugonjwa wa kunung'unika kama sio kulalamika unawatafuna vijana wengi sana wa Kitanzania, yaani kuna fursa ya kuhudhuria ibada inayoendana na mtu lakini bado anakuja JF kulalamika badala ya kwenda moja kwa moja kwenye usharika wake kutoa mapendekezo. Bahati nzuri makanisa yote huwa yanaweka ratiba ya ibada zote na ni kiasi tu cha kuji-adjust kulingana na mahitaji ya lugha yako.Huyu jamaa ana lake jambo,,bahati nzuri leo Upendo Tv walikuwa wanarusha 'Live' ibada ya saa1 asubuhi kutoka Usharika wa Mbezi Beach(KKKT) katika matangazo waliweka bayana kuwa Ibada za saa 1 na saa 4 asubuhi ni za Kiswahili na ya saa 8 alasiri ni ya Kiingereza.Sasa kama 'No English' nenda za Kiswahili