KKKT Mbezi Beach msilazimishe waumini kuabudu kwa Kiingereza

Wakati Taifa lina lengo la kuimarisha matumizi ya lugha yetu kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na elimu wapinzani wa taifa kujikomboa kwenye ukoloni wa lugha na utamaduni wa kigeni wanajibu mapigo kupitia makanisa.

Kama muomini wa KKKT Mbezi Beach sioni mahitaji na ungezeko la ibada na mafunzo ya sunday school kwa Kiingereza.

Ilianza kidogo kwa misa chache sasa kila Jumapili na kwa sikukuu ya chrismas na mwaka mpya. Naona kuna wazee wa usharika wamejaa kasumba ya Kiulaya, binafsi sipendelei jambo hili.

Nina hakika mahitaji ya misa kwa Kiingereza ni madogo sana au hakuna kwa hiyo viongozi wasitulazishe kukosa misa ya pili saa 4.00 asubuhi kwa Kiswahili eti inageuzwa ya Kiingereza.
Ingekua jambo la maana kanisa kuanzisha darasa la lugha ya kiswahili kwa hao waomini wachache badala ya kuwawekea ibada muda muafaka kwa waomini wengi.

Kama ndio usomi mwenyewe ni msomi ngazi ya uzamili ila sipendi kulimbukia utamaduni wa watu wengine.
Hahahapale kqnisani kuna sanduku la maoni
 
Ungeambiwa kwa kiarabu sijui ungesemaje!
 
sisi waslam halituhusu hili maana huwa tunachanganyiwa Quran kwa kiarabu lakini hapo hapo tafsiri inatoka kwa kiswahili hatuna shida.Na endajpo akitokea Shehe mmoja ametokea Arabuni hajui Kiswahili kabisa hapo atatoa mawaidha yake kiarabu pembeni kuna mkalimani anatafsiri haraka igeni utamaduni wa waslam nyie wakristo wenzetu acheni kulalamika huwezi hama kanisa sababu ya lugha.Ukristo na usilam baba yetu ni Ibrahimu
 
Acheni ukuda, hizo ibada zipo katoliki muda mrefu. St Joseph ziko service mbili, 8:45 na 11:45 kila jumapili
 
Back
Top Bottom