KKKT Mbezi Beach msilazimishe waumini kuabudu kwa Kiingereza

Anasoma International School of Tanganyika?

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Wanapataje Ugumu?kwamba mtoto akisoma International School au Englush medium hawezi zungumza Kiswahili fasaha?Wabongo sisi ni shida sana, Colonialism mentality inatuhangaisha sana

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Dunia imebadilika kivipi?acha mindset za ajabu, Kenya wanaongea Kingereza tupu ila kuna watu wana maisha magumu sana hasana hata 100 mfukoni,

Dunia inahitaji vitu kama Networking, Exposure na kadhalika, mbona wachina wanatoka China na hasajui Lugha nyingine na wako Dunia nzima?

Wachina wako Msumbiji na aanapiga biashara ila hawajui Kireno na wanapiga pesa mbaya,

Anaye kudanganya Dunia inahita Kingerez ni nani?

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Si bora hiyo kiingereza utaambulia,mimi ni RC kuna siku mwaka 2006 nilihudhuria ibada St Joseph kuna padre mzee kama Sijasahau jina ni Camilius,akapiga 'show'ya kilatini.Yani sikuambulia hata moja ilikuwa nafata wazee tu wakisimama ,wakipiga goti,wakikaa.
 
Hao wa kuongea kiingereza mbona walishafunga makanisa siku mingi, au wakija bongo ndo wanapata mzuka wa kwenda church..
 
Wajifunze kiswahili sio wenyeji kuwekewa muda wao wa kuabudu ibada ya kizungu. Mbona mwanzo hizo ibada xilikua mchana kwa nini sasa wa cause 'incovinience' kwa wenyeji.
 
Bora ungesema watoto wanasali kingereza kwa lengo la kumudu lugha. Sasa wewe kasumbamtu unafikiri ukisali kwa kingereza ndio utasamehewa ufisadi na mungu? Msisumbue wenzenu kwa mindset zenu za kitumwa.
 
Hiyo Krisimasi ya lini? Kama ya mwaka juu mbona wewe na mimi tulihudhuria ilikuwa ya kizaramo! Unatatizo la kusahau.
 
Bado mnaendeleza ushoga?
 
Kuna misa ngapi?
 
Nadhani mleta uzi sio muumini wa Mbezi beach. Pale kuna misa tatu. Ya sa moja na sa nne ni kiswahili. Ya sa nane mchana ni kiingereza. Pia Sunday school kuna option ya kiswahili na kiingereza. Unachagua unapopamudu
 
mkuu, ungetumia busara sana kulisema hili kwenye jumuiya yako, then wazee wa kanisa wakalichukua kama muhtasari na kuliwakilisha kwenye vikao vya baraza, ujumbe wako ungefika na kujadiliwa kwa kina.....sipingani wa kukubaliana na wewe.....mahali sahihi pa kuanzishia hii hoja yako papo......elewa na hasa kipindi hiki cha xmas...... uchagani (Mlimani - kwa wale tunaoenda kuabudu huko) misa ya pili mara nyingi huendeshwa ki-Chagga.........una haki ya kuchagua ibada kwa lugha yako pendwa.....
 
Bora ungesema watoto wanasali kingereza kwa lengo la kumudu lugha. Sasa wewe kasumbamtu unafikiri ukisali kwa kingereza ndio utasamehewa ufisadi na mungu? Msisumbue wenzenu kwa mindset zenu za kitumwa.
Pole sana mkuu, kila mtu ana uhuru wa kuchagua kilicho ndani ya uwezo wake wether ni utumwa au sio, hata hizi smart phone tunazotumia pia ni utumwa maana ni za wakoloni, hebubtuanze kutengeneza vya kwetu kwanza ndio tukatae vya mabeberu la sivyo mtabaki kuwalaumu mebeberu wakati lugha yao ndio inatawala dunia
 
You have a point mkuu, lakini kwa uchumi wetu huu ambao 60% ya bajeti tunategemea matafifa makubwa ni ngumu kupenya kwenye uchumi wa dunia, lugha yetu ni maarufu tu hapa east africa na hata sio africa nzima, imagine mchina yeye anajitegemea 100% kwenye bajeti yake na elimu yao ni huru na pia soko la dunia linamtegemea mchina kwa asilimia kubwa tu, sio sahihi kujilinganisha na mchina

Kwa sasa, english ni lugha ya dunia, imagine sisi tukapiga marufuku hiyo lugha tukaanza kuzoma kiswahili tu, hivi tunapambana vipi na soko la ajira na uchumi duniani

Hata nafasi za kazi tu hapa bongo, hata za serikali zinataka fluent english speaker, hapa unajiteteaje mkuu?
 
Wanapataje Ugumu?kwamba mtoto akisoma International School au Englush medium hawezi zungumza Kiswahili fasaha?Wabongo sisi ni shida sana, Colonialism mentality inatuhangaisha sana

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Imagine mtoto ameanza shule akiwa na miaka miwili, lugha anayoitumia shuleni ni kingereza tu anashinda shuleni masaa 8 mpaka tisa, mpaka anafika miaka 9 unadhani kiswahili atakua anakijua au anababaisha tu?

Ni sawa na mtoto ambae amezaliwa kwenye jamii wanayoongea lugha ya kikabila, niliwahi kwenda shinyanga, nilikutana na mtoto wa miaka mitano hajui hata neno moja ala kiswahili nilishangaa sana, wenyeji wakaniambia jamii yao wanawasiliana kwa kisukuma tu ndio maana unapoongea kiswahili lazima uwe na mti anawatafsiria wenyeji kwa kisukuma
 
😐😎😐🀨🀨
 
Labda kanisa limejazwa na watu wa kanda fulani wanaojiita wasomi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…