DOKEZO KKKT, ni kwa vigezo gani mlizingatia kumpa Lilian Badi uongozi wa Baraza la Chuo Kikuu cha Iringa?

DOKEZO KKKT, ni kwa vigezo gani mlizingatia kumpa Lilian Badi uongozi wa Baraza la Chuo Kikuu cha Iringa?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Lilian Akijar (Badi) ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Iringa (University of Iringa) kwa sasa lakini Uteuzi wake umeendelea kuzua mijadala ya kimyakimya miongoni mwa viongozi wa KKKT- Dayosisi ya Iringa na jumuiya ya Wasomi kutokana na sababu zifuatazo:-
1. Mwaka 2006 Huyu Lilian Badi aliomba likizo ya miaka mitatu (3) kwenda Masomoni, akaruhusiwa

2. Tangu 2006 hadi 2013 Lilian Badi hakuwahi kuonekana kwenye Kituo chake cha kazi (University of Iringa) licha ya Chuo hicho kuendelea kumlipa mshahara wake hadi Chuo kilipofikia hatua ya kuvunja mkataba wake.

3. Tangu 2006 Hadi Mwaka 2022 wakati anateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Iringa Lilian Badi alikuwa hana mawasiliano yoyote na uongozi wa Chuo hicho na haijulikani kama alifanikiwa kuipata hiyo PhD aliyodai anaenda kusomea,

4. Bado wanajumuiya ya Wasomi na Dayosisi tunahoji, inawezekanaje mtu aliyekuwa akila Mshahara wa bure wa Chuo kwa zaidi ya miaka mitano na ambaye CV yake Ina mashaka akateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo chenye watu waliobobea kwenye taaluma, Kuna madokta,maprofesa na watu waadilifu kuliko yeye aliyekimbia chuo hicho kwa kisingizio cha kwenda Masomoni!! Hii sio sawa.

5. Mbali na hayo, uwezo wake wa kuliongoza Baraza la Uongozi wa Chuo Kikuu cha Iringa unaonekana kuwa ni mdogo na hatari yake ni kwamba Chuo kipo hatarini kupoteza sifa yake.

Wote tunafahamu kuwa sifa ya Chuo Kikuu Chochote Duniani hutegemea sana sifa za watumishi wake, watendaji wake au viongozi wake, kwa hili la Lilian Badi ambaye hata yeye mwenyewe anaogopa kujiita Dokta litazorotesha sana Maendeleo ya Chuo Kikuu cha Iringa iwapo hatua za haraka za kukinusuru Chuo hazitafanyika.

Aidha, taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa Suala la Ukabila limechangia uteuzi wake, kwani Askofu wa Dayosisi ya Iringa (KKKT) Blaston Gavile na Lilian Akijar (Badi) ni kabila Moja, wanatoka Kijiji kimoja, ukabila haujawahi kuiacha Taasisi salama.

Mbali na ukabila, taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Lilian Akijar (Badi) ni mtoto aliyelelewa na Chuo hicho tangu wakati anasoma chuoni hapo na kwamba Askofu wa sasa wa Dayosisi ya Iringa Blaston Gavile ambaye ndiye aliyemteua Lilian Akijar amekuwa akinufaika tangu zamani kutoka kwa Lilian Badi, na kwamba hata Askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo askofu Mdegela naye amekuwa na Maslahi ya muda mrefu na Lilian Badi jambo linalotia mashaka kwamba uteuzi wailian Badi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Iringa nyuma yake kuna Maslahi ya Maaskofu hao wawili.

6. Mpaka sasa Lilian Badi hajawahi kurejesha fedha za mshahara aliokuwa akiupokea BURE kwa zaidi ya miaka mitano alipokuwa amekikimbia Chuo hicho, hii haileti picha nzuri au mfano wa kuigwa kwa kiongozi, vinginevyo alipaswa kurejesha pesa/mishahara aliyokuwa akiipokea Bure katika kipindi chote ambacho hakuwepo chuoni hapo bila taarifa yoyote.

7. Kama mtu alikikimbia Chuo kwa kisingizio cha kwenda masomoni Hadi kupelekea mkataba wake kusitishwa anakuwa ndio Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Kikuu cha Iringa hivi atawezaje kuwa na sifa za Uongozi kuliongoza Baraza la Chuo! Huku kubebana kutaligharimu sana Kanisa.

Documents mbalimbali zinaonyesha jinsi Chuo Kikuu cha Iringa kilimvumilia kwa utovu wa nidhamu wa hali ya juu wa kuomba ruhusa na kupotea mazima lakini yeye na watu walio nyuma yake wameshindwa kukiheshimu Chuo hicho na jumuiya ya Wanachuo, hiyo ni dharau kubwa, hivi Lilian angekuwa serikalini angeweza kufanya madudu hayo?Yani serikali ikupe likizo ya miaka mitatu,alafu wewe ukae miaka 6 bila mawasiliano na serikali,iendelee kukulipa,Hadi inakufukuza kazi alafu inakurudisha tena! Haya mambo tunayaona kwenye makanisa yetu tu,ndio maana hatuendelei,

Hivi, Lilian angekuwa na mkataba na taasisi ya kanisa katoliki wangefanya upuuzi wa kumteua mtu aliyeonyesha dharau kubwa kiasi kama alivyofanya Lilian Badi!! Jibu ni hapana.

Naomba viongozi wa Dayosisi ya Iringa na jumuiya ya Chuo Kikuu cha Iringa mlitafakari jambo hili na kuchukua hatua za haraka kukinusuru Chuo chetu, vinginevyo hatutawaelewa.

Inapofikia hatua ya waumini na viongozi wa Dayosisi kufanya maandalizi ya kulifikisha suala hili kwa Mkuu wa Kanisa pamoja na Takukuru ili mwafaka upatikane itakuwa ni aibu kwa kanisa na Chuo Kikuu cha Iringa, something must be done
View attachment 3284110
View attachment 3284207
Sio kila mtu anafanyakaz katika mtiririko wa kawaida mkuu. Wengine ni kaz maalumu jiongeze. Unawaona hawapo lakin wapo
 
Back
Top Bottom