KKKT sadaka za marehemu wapewe wafiwa baada ya ibada, mambo ya tutakuja mkirudi yafe

KKKT sadaka za marehemu wapewe wafiwa baada ya ibada, mambo ya tutakuja mkirudi yafe

Tutofautishe neno sadaka na mchango. Sadaka inaandaliwa na inaambatana na maombi ya mtoa sadaka siku ya ibada. Hii onatakiwa iende kanisani (labda Msikitini pia) ifanyiwe mchakato kama sadaka nyingine. Yawezekana muda wa ibada madhehebu mengine yanakaa pembeni kupisha utaratibu wa ibada.
Baada ya ibada weka kikapu watu watoe mchango.
 
Huu nao ni utapeli.
Kama kusingetokea msiba wangezipata wapi?
 
yaani mpaka mtu AFE ndo mchukue sadaka?
Asingekufa?
Nyie subirini sadaka zenu za jumamosi na jumapili.
Vingenevyo watu watawahisi kuwa MNAPENDA wafe ili mkusanye sadaka za marehemu.
Kuna wakati marehemu anaondoka anaacha madeni hizo sadaka zingesaidia
Kwani sadaka maana yake ni nini, nadhani ni sehemu ya ibada kwaiyo kuziacha kwa familia ya marehemu ni hiyari na sio lazima. Na ndio maana kuna michango ya rambirambi kwaajili ya familia.
 
Poleni sana marehemu watarajiwa mnaosoma hapa

Vizuri tukaelimisha makanisa ndugu zenu wasiteseke mnapotangulia.

Juzi tulikuwa msiba mmja kanisa moja kmr kumwaga mama yetu mmoja.

Watu walishiriki kwa kutoa sadaka baada ya sadaka mch anasema sadaka hizi tutaleta kwa mume wa marehemu akirudi iliumiza wengi sana.

Hata waliposhauriwa wafiwa wanahtaji ziwasaidie safarini waligoma kutoa .Sasa unajuaje atarudi wewe ni Mungu.

Ushauri makanisa yote.

Sadaka wapewe wafiwa siku ileile mtafanya watu washinde bar kuuluzia kama mda wa kuaga umefika.

Tuombe

Sala ya bwana

Neema ya bwana wetu

Mungu awape mwisho mema mnaosoma na nyie msisndikize tu siku moja msisndikize na muwe kwenye kitabu cha uzima wa milele

Amen
Kwani sadaka maana yake nini?
Sadaka ni pesa inayotolewa kwenye ibada.
RAMBIRAMBI JE?
Ni pesa ya kuwafariji wafiwa.
Je rambirambi na sadaka ni sawa?
Je ni wajibu wa kanisa kukusanya rambirambi?
 
yaani mpaka mtu AFE ndo mchukue sadaka?
Asingekufa?
Nyie subirini sadaka zenu za jumamosi na jumapili.
Vingenevyo watu watawahisi kuwa MNAPENDA wafe ili mkusanye sadaka za marehemu.
Kuna wakati marehemu anaondoka anaacha madeni hizo sadaka zingesaidia
Hamna ibada ambayo haiendani na sadaka. Hata ibada za matambiko, na hata ibada mnazofanya na waganga wenu mnapelekea sadaka, je kwanini mnakasirika na sisi tukimtolea Mungu wetu kwa furaha na moyo wa kupenda?
 
Kwani sadaka maana yake ni nini, nadhani ni sehemu ya ibada kwaiyo kuziacha kwa familia ya marehemu ni hiyari na sio lazima. Na ndio maana kuna michango ya rambirambi kwaajili ya familia.
Sadaka haitakiwi kupewa familia ya marehemu. Familia itapewa rambirambi. Kiroho, sadaka ni mali ya Mungu, Mungu ndio ibada yenyewe. Hata mkienda kutambika bamuendi mikono mitupu, pia mkienda kwa waganga hamuendi kinyonge, iweje mnataka kumpora Mungu haki yake?
 
Sijaelewa. Huyo mume yuko wapi?
My prophet
1665198756541.png
 
Hamna ibada ambayo haiendani na sadaka. Hata ibada za matambiko, na hata ibada mnazofanya na waganga wenu mnapelekea sadaka, je kwanini mnakasirika na sisi tukimtolea Mungu wetu kwa furaha na moyo wa kupenda?
Asingekufa sadaka mngepata wapi?
 
Back
Top Bottom