KKKT sadaka za marehemu wapewe wafiwa baada ya ibada, mambo ya tutakuja mkirudi yafe

Tutofautishe neno sadaka na mchango. Sadaka inaandaliwa na inaambatana na maombi ya mtoa sadaka siku ya ibada. Hii onatakiwa iende kanisani (labda Msikitini pia) ifanyiwe mchakato kama sadaka nyingine. Yawezekana muda wa ibada madhehebu mengine yanakaa pembeni kupisha utaratibu wa ibada.
Baada ya ibada weka kikapu watu watoe mchango.
 
Huu nao ni utapeli.
Kama kusingetokea msiba wangezipata wapi?
 
yaani mpaka mtu AFE ndo mchukue sadaka?
Asingekufa?
Nyie subirini sadaka zenu za jumamosi na jumapili.
Vingenevyo watu watawahisi kuwa MNAPENDA wafe ili mkusanye sadaka za marehemu.
Kuna wakati marehemu anaondoka anaacha madeni hizo sadaka zingesaidia
Kwani sadaka maana yake ni nini, nadhani ni sehemu ya ibada kwaiyo kuziacha kwa familia ya marehemu ni hiyari na sio lazima. Na ndio maana kuna michango ya rambirambi kwaajili ya familia.
 
Kwani sadaka maana yake nini?
Sadaka ni pesa inayotolewa kwenye ibada.
RAMBIRAMBI JE?
Ni pesa ya kuwafariji wafiwa.
Je rambirambi na sadaka ni sawa?
Je ni wajibu wa kanisa kukusanya rambirambi?
 
Hamna ibada ambayo haiendani na sadaka. Hata ibada za matambiko, na hata ibada mnazofanya na waganga wenu mnapelekea sadaka, je kwanini mnakasirika na sisi tukimtolea Mungu wetu kwa furaha na moyo wa kupenda?
 
Kwani sadaka maana yake ni nini, nadhani ni sehemu ya ibada kwaiyo kuziacha kwa familia ya marehemu ni hiyari na sio lazima. Na ndio maana kuna michango ya rambirambi kwaajili ya familia.
Sadaka haitakiwi kupewa familia ya marehemu. Familia itapewa rambirambi. Kiroho, sadaka ni mali ya Mungu, Mungu ndio ibada yenyewe. Hata mkienda kutambika bamuendi mikono mitupu, pia mkienda kwa waganga hamuendi kinyonge, iweje mnataka kumpora Mungu haki yake?
 
Hamna ibada ambayo haiendani na sadaka. Hata ibada za matambiko, na hata ibada mnazofanya na waganga wenu mnapelekea sadaka, je kwanini mnakasirika na sisi tukimtolea Mungu wetu kwa furaha na moyo wa kupenda?
Asingekufa sadaka mngepata wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…