KKKT wamtaka rais Magufuli akamilishe Katiba Mpya

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
ASKOFU mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.

Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake, Himidi Sagga, katika ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa.

Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote na

kwa kufanya hivyo, ni faraja kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kweli nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa moyo na rais na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema Askofu Gaville.

Hata hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika ya dini kwakuwa baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa kuendeleza elimu kupitia vyuo vya ufundi.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto masikini wapate haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi.

Chanzo: Mtanzania
 
magazeti mengine bhana, ina maana huyo askofu wa iringa ndiye msemaji wa kkkt?!
Hayo ni maoni yake binafsi bila kulihusisha kanisa zima.
 
Maoni yako yana ukakasi wa udini na ukabila, Tanzania tulishatoka huko, unashangaza kurudi Misri wakati tupo Kanaani
 
ASKOFU mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.

Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake, Himidi Sagga, katika ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa.

Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote na

kwa kufanya hivyo, ni faraja kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kweli nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa moyo na rais na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema Askofu Gaville.

Hata hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika ya dini kwakuwa baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa kuendeleza elimu kupitia vyuo vya ufundi.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto masikini wapate haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi.

Chanzo: Mtanzania
Hapo kwenye alimu mhhhh!! Nafikiri walipe tu kodi maana shule za madhehebu ya dini ada zao ni kubwa kuliko hata za watu binafsi japo shule zao hujengwa kwa kusaidiwa na sadaka za waumini... Sioni kama ni msaada bali huwa biashara.
 
Katiba ya Warioba ndo inafaa Kwa 100% na sio Ile ya Chenge na Sita
 
Alikwishasema ananyoosha nchi kwanza kwa hiyo àskofu atulie kwanza anyooshwe
 
KKKT inaburuzwa na ASKOFU SHOO ambaye kwanza ni mangi pili ni TeamLowassa, Hakuna cha katiba hapo wala dini ni KUTAFUTA ULAJI TU wa NORTH POLE
Kwa mawazo mgando kama haya ndio maana unakosa hata hela kidogo!
Unabaki kukaa getto na wanaume wenzio halafu unakuja kuomba mkopo jf!
 
Nimepangisha mamangi hapa kwangu na nimewaruhusu mpaka wanafuga kuku licha ya kuwa ni mabaguzi kupindukia
 
Jichunge sana mkuu hizo njaa njaa zako za kuja kuomba mkopo kwa watu usio wa fahamu utakuja kupakatwa!
Shauri zako
Mimi ndo napakata mangi tena sina kibamia, kama uko tayari PM
 
Back
Top Bottom