KKKT wamtaka rais Magufuli akamilishe Katiba Mpya

KKKT wamtaka rais Magufuli akamilishe Katiba Mpya

Mimi ndo napakata mangi tena sina kibamia, kama uko tayari PM
Wenzio wanauza kofia za chama kule kariakoo jombaaaa!
Wewe mwanaume unakuja kulia lia huku?
Huna adabu we!
 
Rais wa jamhuri ya muungano dkt john pombe Joseph magufuli ktk kampeni zake za Lusaka urais 2015 hakuwahi kutamka kuwa atakamilisha /ataendelea na ukamilishaji wa katiba.
Mimi nijuavyo na ninavyofikiria ,Mh Rais john pombe Joseph magufuli atashughulika na ukamilishaji wa katiba Mpya kuanzia 2021 hadi 2025 . ktk miaka hii mitano,yeye amejikita na masula ya kusimamia nidhamu ya watumishi,kurekebisha uchumi, watumishi hewa , vyeti feki n.k.
 
Katiba mpya si kipaumbele kwa sasa,kama watu waliitumia nafasi vibaya nafasi waliopewa kutuletea katiba,wasifikirie nafasi huja mara mbili.
Subirini tufyeke mafisadi kwanza
 
Baba Askofu unayo mawazo mazuri sana lakini hayo mawazo yako hayawezi kutekelezwa na mtu wa aina hiyo. Yeye anayo mipango yake kuhakikisha chatou panakuwa makao makuu ya nchi
 
ASKOFU mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, amemuomba Rais Dk. John Magufuli kumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya ulioachwa na mtangulizi wake.

Akizungumza baada ya kuwekwa wakfu Askofu Gaville na msaidizi wake, Himidi Sagga, katika ibada iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya Msingi, Gangilonga, alisema Wakristo na Watanzania kwa ujumla wana imani kubwa na Serikali ya Dk. Magufuli na ni matarajio yao kwamba mchakato wa kuandika Katiba mpya utamalizwa kama lengo lilivyokuwa.


Askofu huyo alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya siasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Katika ibada hiyo, Askofu Gaville alieleza kuwa wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dk. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote na

kwa kufanya hivyo, ni faraja kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kweli nasema nchi yetu ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, tunatiwa moyo na rais na Serikali yake tunapoona wanatetea wanyonge,” alisema Askofu Gaville.

Hata hivyo, askofu huyo aliiomba Serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika ya dini kwakuwa baadhi ya kodi wanazolipa ni kwa kuendeleza elimu kupitia vyuo vya ufundi.

“Katika kuunga mkono jitihada za Serikali, kanisa linasaidia watoto masikini wapate haki yao ya elimu, tunaomba Serikali isituingize katika kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi.

Chanzo: Mtanzania

'Ndugu zangu Walutheri..." By Lowassa, 2015
 
Mkitaka katiba mbovu kuliko tunayoikataa turuhusu utawala huu utunge katiba
 
Nchi za kipeasant zina matatizo makubwa....fikiria ni kiasi gani serikali imepoteza katika mchakato wa katiba mpya halafu hakuna matokeo ya huo mchakato! Leo tunakuja mbele ya wananchi na kuwaaminisha kwamba fedha nyingi zimeibiwa na ACASIA ndo maana hakuna madawa hospitalini....vipi hizo ambazo serikali imezipoteza bila kazi yoyote...wakati mwingine Magu asisingizie mafisadi kwamba ndo tatizo....serikali nayo pia inawafisadi wananchi wake...Billions of money zinapotezwa hivihivi kwenye mchakato wa katibu...bila faida yoyote!
 
Back
Top Bottom