Klabu bingwa barani Afrika,ES Setif imevuliwa ubingwa kwa kuchapwa mabao 2-0 na El Merreikh ya Sudan jijini Khathoum. Setif walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza.
El Merreikh imetinga hatua ya nusu fainali na sasa itaivaa TP Mazembe ya DR Congo. Imefika hatua hiyo baada ya kufika hapo mwaka 1975.