Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Kufuatia ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Galaxy hivi punde na kimahesabu, ASEC Mimosas wametinga hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa barani Afrika.
Hadi sasa, ASEC wamefikisha alama 10 huku ikibaki michezo miwili. Simba wana alama 5, Galaxy alama 4 na Wydad alama 3.
Kimahesabu, Simba au Galaxy tu ndio wanaoweza kufika alama 10 au zaidi huku wakiwa na mechi moja baina yao. Wydad kama atashinda michezo yake iliyobakia atakomea alama 9.
Hata kama ASEC watapoteza michezo yao miwili iliyobakia bado watakuwa wameshafuzu kwakuwa wanaoweza kuwafikia ni Simba au Galaxy tu.
Kongole ASEC Mimosas, mabingwa wa Ivory Coast!