Klabu Bingwa Barani Afrika: Waarabu Esperance na Wydad Casablanca watinga fainali

Klabu Bingwa Barani Afrika: Waarabu Esperance na Wydad Casablanca watinga fainali

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa barani Afrika, Esperance ya Tunisia na Wydad Casablanca ya Morocco wametinga fainali ya michuano tajwa baada ya kupata suluhu kwenye mechi zao za leo zilizoisha hivi punde ugenini.

Esperance ilipambana na TP Mazembe ya DR Congo huku Wydad Casablanca ikipepetana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Katika michezo ya awali, Esperance walishinda 1-0 huku Wydad wakiibuka na ushindi wa 2-1.

Wote leo, wakiwa ugenini wamepata matokeo ya 0-0 yaliyowavusha kuwapeleka fainali. Esperance wapo kwenye nafasi ya kutetea kombe la michuano hiyo ambalo msimu uliopita walilitwaa wakiwabwaga Al Alhy ya Misri.
 
Tusubiri msimu ujao, lakini tunakosea wapi?
Tunakosea mambo matatu. Mosi, usajili na kikosi hufanywa na viongozi badala ya benchi la ufundi. Pili, maandalizi kabla ya michuano huwa finyu na zaidi midomoni kuliko uhalisi. Tatu, kufungwa au kutoa sare uwanja wa nyumbani. Hayo ni kwa timu ya taifa na klabu zinazotuwakilisha kimataifa.
 
Nimeangalia game ya Wydad vs Mamelodi 1st leg pamoja na game ya leo 2nd leg hakika fedha ndio kila kitu!! Watu wamewekeza haswa hizi timu ni level nyingine!!. Hili tusogee yapaswa ligi yetu iwe na udhamini wa kutosha timu ziweze kujiendesha vizuri tuweze kuona ushindani wa kweli!!
 
Tusubiri msimu ujao, lakini tunakosea wapi?
Susls lako ni zuri na Lina chonga Kama msumeno!!
Kwanza nawapa ArabAfro Hongera nyingi Sana maana vikombe vinabaki Ktk Vantage zao!!
Jibu :- Bajeti yote ya michexo ilenge kuwanufaisha wachezaji/Wana michezo na siyo Viongozi na wasimamizi wa michezo!!
Hapo tutazika wachezsji uwanjani kufa na kupona!!
Good luck next yrs
 
Back
Top Bottom