Klabu imevunja mkataba na staa wa Cameroon baada ya kugundua kuwa ana HIV

kamtu33

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Posts
998
Reaction score
409
Moja kati ya habari zinazo-trend kwa siku ya leo August 29 2016 katika soka ni hii ya klabu Al Ittihad Alexandria ya Misri kutangaza kuvunja mkataba na nyota wa kimataifa wa Cameroon Samuel Nlend kutokana na kugundua kuwa nyota huyo ana HIV.

Al Ittihad Alexandria imevunja mkataba na Samuel Nlend mwenye umri wa miaka 21 kutokana na kupimwa kwa nyota huyo na kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi, maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni siku nne zimepita toka nyota huyo asaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu hiyo.


Samuel August 24 2016 alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu ya Al Ittihad Alexandria, Samuel amewahi kuichezea timu ya taifa ya Cameroon mechi tano, hata hivyo hakuna sheria yoyote itakayomzuia staa huyo kupata kibali cha kucheza soka katika nyingine licha ya kugundulika kuwa na virusi vya ukimwi.
 
Hawa waarabu hawana maana kabisa kana kwamba wao ni watakatifu saaana
 
Picha hii ya wakati akisaini inaonesha alikua kakonda for me hawezi kucheza mpira ila majibu ya vipimo kutangazwa hadharani ni kosa.
 

Attachments

  • IMG_20160829_201533.jpg
    50.9 KB · Views: 81
Maskini pole yake, ila kumtangaza adharani kama wamemwalibia
 
Mkuu Magic alicheza kwa muda lakini baadhi ya wachezaji wakiongozwa na Karl Malone hawakuwa comfortable kucheza na Magic. Kwanza ilikuwa minong'ono ya timu nyingine na minong'ono hiyo ikaingia mpaka ndani ya LA Lakers na hata baadhi ya wachezaji kuonyesha wasiwasi wa kufanya mazoezi na Magic katika maandalizi ya mechi zao. Hatimaye minong'ono hiyo kuwa public na kumfikia Magic ambaye aliamua kuretire.

Niliangalia document yote kuhusu hii issue na kwa kweli inasikitisha sana lakini nilifurahishwa sana na Magic na mkewe, mkewe hakuparticipate kwenye hiyo documentary lakini Magic alielezea mchango wake mkubwa wa yeye kuona thamani ya kuendelea kuishi baada ya kumruhusu mkewe aondoke na mkewe kugoma kuondoka na kutaka kuendelea na ndoa yao pamoja na yeye kuwa muathirika..



Unyanyapaa wa Waarabu huo.

Magic Johnson kapiga kikapu miaka kadhaa huku ana HIV, na mpaka leo anadunda. Huku watu ambao hawakuwa na HIV wanakufa kila siku.

Kwa upande mwingine HIV/AIDS is real people.
 

Asante kwa post.

Lakini Magic hakukataliwa na klabu, klabu ilim support. Ni mambo ya wachezaji binafsi tu. Tena kumbuka siku zile hamna dawa, HIV was like a death sentence.

Sasa ukiangalia leo kuna dawa kibao, Wamisri wamemkataa huyu kwa HIV wakati hata hamna clause hiyo.

Hapo utaona tofauti ya Muarabu na Mnyamwezi.
 
Unyanyapaa upo kweli..Inasikitisha kumtangaza mtu status yake in public.Hapo ethics imekua violated
 
Waarabu kweli nuksi! Jamaa amtafute Tundu Lisu wakaifungulie hiyo club mashtaka kwa huo udhalilishaji na alipwe hela kwa kuvunjiwa mkataba!!

Duh.....................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…