Klabu ipi maarufu zaidi Afrika ligi ya England?

Klabu ipi maarufu zaidi Afrika ligi ya England?

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677

Kwa mashabiki wa soka barani Afrika, Ligi Kuu ya England ndio sasa basi, ndio mwisho wa kila kitu, ndio eneo lao la maabadi. Nembo hii ya kimataifa katika soka inafuatiliwa na zaidi ya watu bilioni moja kote duniani na watu milioni 260 kati ya hao wapo barani Afrika.

Huku msimu mpya wa mwaka 2015-16 ukianza, majumba ya starehe na mikahawa kutoka Cape Town hadi Cairo itakuwa ikijiandaa kukidhi mahitaji ya mashabiki wengi watakaokuwa wakifika tayari kushudia kipute hicho kwenye runinga kubwa kubwa zilizotundikwa ukutani.

Lakini ni timu gani ambayo ni maarufu zaidi katika bara hili?

Huenda tusiweze kabisa kujibu swali hili kikamilifu, japo utafiti uliofanywa na twitter unatupa sura ya wastan, kwa kukadiria idadi ya jumla ya watu katika kila taifa ambao wanafuata anwani rasmi ya timu za ligi kuu England kwenye twitter na kisha kuziainisha tarakimu hizo katika asilimia kwa kila kilabu.

Magharibi

Hapana shaka Chelsea ndio maarufu zaidi katika eneo hili. Hutoweza kuzungumzia Ligi kuu nchini Englan katika eneo la Magharibi mwa Afrika bila kuwazia Didier Drogba, Solomon Kalou, Samuel Eto'o, Victor Moses, Michael Essien na John Mikel Obi, wote ni wenyeji wa Afrika ya Magharibi ambao wameichezea The Blues.

Hata hivyo, Drogba ndiye mashuhuri zaidi kutokana na mafanikio yake nje na ndani ya uwanja. Hapana shaka kwamba alikuwa mshambulizi mtajika klatika klabu hiyo, akifunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti na kuisaidia Chelsea kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa mwaka 2012, na pia kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Magharibi kufunga jumla ya mabao 100 katika Ligi kuu England mwaka huo.

Kadhalika Drogba anaheshimika sana nyumbani Ivory Coast kwa juhudi zake za kueneza amani baada ya mzozo ulioibuka kati ya mwaka 2010-2011, na ameanzisha wakfu wake kuimarisha afya na elimu katika taifa hilo.
Mashariki

Chaguo la wengi katika eneo la Afrika Mashariki ni rangi nyekundu ya Arsenal. Umaarufu mkubwa zaidi wa the Gunners katika eneo hili unaweza kuwa ulitokana na dhana ya kuwa timu 'isiyoweza kushindwa', baada ya timu hiyo kuvunja rekodi katika msimu wa mwaka 2003-04 kwa kunyakuwa ligi bila kupoteza mechi yoyote, ilicheza mechi 49 bila kupoteza yoyote.

Mafanikio ya wachezaji wa Kiafrika kama vile Nwankwo Kanu, Emmanuel Adebayor, Kolo Toure na Lauren ilifanya Arsenal kuwa maarufu hata zaidi. Kanu bila shaka ndiye sababu ya Arsenal kupata umaarufu mkubwa nchini Nigeria.

Jambo la kushangaza ni kwamba Afrika Mashariki imepata kutuma mchezaji mmoja pekee katika Ligi Kuu nchini England - mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya na kilabu ya Southampton Victor Wanyama.

Kusini

Sio jambo la kushangaza kuwa Manchester United ndio timu mashuhuri zaidi katika eneo la kusini mwa Afrika.
Manchester United ndio timu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu England, baada ya kushinda jumla ya mataji 13 tangu ligi hiyo ianze mwaka 1992.

Pia Manchester United iliwahi kumsajili mmoja wa wachezaji mashuhuri zaidi wa Afrika Kusini, Quinton Fortune, aliyewachezea Red Devils kwa kipindi cha miaka saba.

Fortune pia ni mmoja wa wachezaji wengi wa zamani wa Man U wanaozuru eneo hilo kila mwaka kutangaza timu hiyo. Afrika kusini ilikuwa nchini ya kwanza barani Afrika kuwa na chama cha wapambe wa Manchester United.
Kaskazini

Kwa watu wa Afrika Kaskazini Arsenal ndio timu maarufu zaidi. The Gunners inawakilishwa vilivyo nchini Morocco, Algeria na Tunisia.

Vyama vya wapambe wa klabu hiyo katika mataifa haya vimesaidia kuipa klabu hiyo umaarufu kupitia mashindano kama vile mbio za kila mwaka za "Be a Gunner. Be a Runner".

Lakini nchini Misri, ni Chelsea ndio inayotawala - hii ni baada ya timu hiyo kumnunua Mohamed Salah kwa kima cha dola $17m aupauni £11m mwezi Januari mwaka 2014.

Timu za Ligi Kuu England zenye ufuasi mkubwa zaidi kwenye Twitter:
Arsenal - wafuasi milioni 6.14
Chelseafc - wafuasi milioni 5.92
manutd - wafuasi milioni 5.73
@LFC - wafuasi milioni 4.64
@MCFC -wafuasi milioni 2.59


Source: BBC

 
Bolton wonderers japo ilishuka daraja
 
Siamini katika huo utafiti.
Sio rahisi Arsenal kuwa na mashabiki wengi hivyo.
 
ww ndio huamini lakn ndio ukweli wenyewe! gunners for life! kama siyo kuibuka kwa chelsea miaka ya karibuni no. ya mashabiki wa arsenal inge-double hapo. mashabiki wengi wa chelsea na man city wamechepuka toka arsenal
 
Tafiti za uongo hizo, Arsenal ni miongoni mwa timu ambazo hazina mashabiki wengi barani Afrika.
 
Watu wengne ni wavivu wa kufikiri,si ufungue account zao za twitter ushuhudiee piaa!
 
Unazani ukijikuta ww na marafiki zako mnashangilia man u/Chelsea/Liverpool mnazani ndo mko wengi....! Wala sikatai kwa upande wa east Africa km mtu unafatilia matukio ya soka england utajua kabisa kuwa arsenal ndio team inayoongoza kwa mashabiki
 
Arsenal ndio kubwa lao...anayepinga hana akili timamu.
 
Utafiti feki ,kwa africa 80.7% ya watumiaji wa internet ni watumiaje wa facebook na ndio social netwerk inayoongoza kutumiwa na waafrica. wakati twitter inashika nafasi ya 4 kwa africa. sasa hapo facebook au twitter ipi ilikuwa sahihi kutumika?
 
Sasa ifanyike tafiti za Asia, utakuta "wote" ni Manu, huko Manu ni kama Mungu!
 
ww ndio huamini lakn ndio ukweli wenyewe! gunners for life! kama siyo kuibuka kwa chelsea miaka ya karibuni no. ya mashabiki wa arsenal inge-double hapo. mashabiki wengi wa chelsea na man city wamechepuka toka arsenal

Washabiki waliochepuka wanarudi vere soon njia kuu.
 
utafiti uliofanywa na twitter unaonyesha idadi ya mashabiki wa hizi timu! sema timu yenye followers wenye kwenye twitter. hebu ondoa biased opinion yako hapa. arsenal iwe na mashabiki wengi kuliko red army with trident! maajabu
 
utafiti uliofanywa na twitter unaonyesha idadi ya mashabiki wa hizi timu! sema timu yenye followers wenye kwenye twitter. hebu ondoa biased opinion yako hapa. arsenal iwe na mashabiki wengi kuliko red army with trident! maajabu

Ndio hivyo sasa, basi tumia hata JF na majukwaa ya timu uone jukwaa lipi linachanja mbuga kwa comments, washabiki wengi na haters wengi!
Sijawahi ona mshabiki wa Manu anaipenda Arsenal, yaani hata wakiwa wanahitaji msaada wa Arsenal ishinde waweze nufaika na ushindi wa Arsenal KAMWE hawashabikii Arsenal, sijui Wenger aliwafanyaga nini? Duh!
Ila nafikiri ile record ya invincible inawauma sana watu.
 
Ndio hivyo sasa, basi tumia hata JF na majukwaa ya timu uone jukwaa lipi linachanja mbuga kwa comments, washabiki wengi na haters wengi!
Sijawahi ona mshabiki wa Manu anaipenda Arsenal, yaani hata wakiwa wanahitaji msaada wa Arsenal ishinde waweze nufaika na ushindi wa Arsenal KAMWE hawashabikii Arsenal, sijui Wenger aliwafanyaga nini? Duh!
Ila nafikiri ile record ya invincible inawauma sana watu.

Na hakuna wa kuivunja sasa!
 
Back
Top Bottom