Klabu ya African Lyon kuhamia mkoa mwingine, kufuatia kukosa mashabiki wa kuiunga mkono katika jiji la Dar

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Zamunda Kangezi, anapambana kuihamisha timu hiyo kutoka Dar es salaam kwenda mkoa mwingine kwa sababu ya kukosa mashabiki wa kuiunga mkono katika jiji la Dar es salaam.

"Huwezi kuwa na timu Yatima, aliyeanzisha timu alikosea, umewahi kusikia timu haina mashabiki? Sio rahisi kuendesha timu bila mashabiki ndo maana tunataka tuhame Dar es salaam".

"Tutabadilisha Jina, na kuna mikoa mitatu tunaongea nayo ikiwemo Kilimanjaro, lakini tutaona ni mkoa gani halafu tunahamia moja kwa moja hatuendi kwa michezo ya ligi, tukiondoka haturudi tena, tunataka tuwe na mji wetu, Dar ni pagumu sana Simba na Yanga wameshachukua mji".

"Siwakimbii Simba na Yanga lakini inabidi ujue maana ya 'African Lyon' African ni Yanga Afrika na Lyon ni Simba, kwahivyo walikuwa wanataka tuwaunganishie mashabiki tukae katikati lakini mpango huo haukufanikiwa". Amesema Rahim
 
Paragraph ya mwisho, ndo mwisho wa matatizo. Ni ya kufikirika mno!
 
Wachukue ubingwa wa TPL, hapo ndo watapata mashabiki lukuki..!
 
kweli dar pagumu kwenu... bora hata mpeleke Mara
 
Nawashauri watangulie Dodoma hawatajuta kwa sasa.
 
Makonda alisema atakayebakia Daslam mwanaume naona Lyon anakimbia

Aende Arusha amini watapata mashabiki waende mikoa ambayo hakuna timu ligi kuu kama Arusha,Dom,klm,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…