Zanzibar ni nchi, hatutakiwi kuwa na hasira katika jambo hili lililo wazi.
Tanganyika nayo itafute namna ya kutangaza urithi na vivutio vyake badala ya kulalama na kulia .
Habari kwa kina :
Chelsea FC Washirikiana na Serikali ya Zanzibar Kuinua Utalii
Na
Ripoti ya Hoteli ya Afrika, 2024
Chelsea: Kukuza Utalii na Maendeleo ya Soka Zanzibar
Lengo kuu ni la kuimarisha sekta ya
utalii Zanzibar sambamba na kukuza maendeleo ya soka katika visiwa hivyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha vyuo vya soka ndani ya Visiwa hivyo.
Bw. Barnes Hampel na timu yake wanapanga ziara ya Tanzania kukutana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Damas Ndumbaro. Ajenda yao ni pamoja na kuchunguza mipango ya maendeleo ya michezo, kuimarisha athari za ushirikiano katika utalii na michezo ya ndani.
Mratibu wa Chelsea FC nchini Tanzania, Bw. Mohamed Reza Saboor, alithibitisha lengo la wajumbe hao kupata wasaa wa mazungumzo na
Rais Samia Suluhu Hassan, wakiangazia wigo mpana wa mashirikiano yao.
Ushirikiano huu unaashiria mtazamo wa kufikiria siku za mbele zijazo, unao fungamanisha uwezo wa soka wa kimataifa na uchangamfu wa kitamaduni na kimichezo wa Zanzibar.
Kuhusu Chelsea Football Club
Klabu ya Soka ya Chelsea , yenye makao yake mjini London, inasimama kama klabu tajwa maarufu katika ulimwengu wa soka. Ikijulikana kwa historia na mafanikio yake tele, klabu hiyo imekuwa mstari wa mbele katika mashindano ya ndani na kimataifa.
Ni dhahiri katika ushirikiano wao wa hivi karibuni na serikali ya Zanzibar, uonesha dhamira ya maendeleo ya michezo na ushiriki wa jamii. Kama taasisi kuu ya soka, Chelsea inaendelea kuacha alama kwenye mchezo huo wa soka , ikivuka mipaka na kuwaunganisha mashabiki duniani kote