Klabu ya JS Kabylie ya Algeria imekamilisha ujenzi wa uwanja wake

Sio sahihi kufananisha Simba na Yanga na Js kablylie

Hiyo Kabylie sio club ndogo. Imeshawai kutwaa Caf champions league

Mamelodi sundown hana tofauti na Kabylie kimafanikio ya soka.
 
Huu ndio ukweli, ni mechi ngapi mashabiki wana jaa uwanjani,? uwanja ni hasara hizo pesa ni bora kuwekeza kwenye kukuza watoto na training facilities ili kupingunza sajiri za gharama kubwa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kunielewa una GB ndogo kichwani

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kamasi lililooza.

Kumiliki uwanja maana yake unapungua gharama za uendeshaji. Unakodisha uwanja unalipia hosteli, uwanja wenyewe.

Mapato ya mlangoni Ni yako.

Maana yake utakuwa na uwanja wwnye facilities zote una uhakika was timu Kufanya mazoezi kwa utulivu.

Watakuwa na jiko na wataalamu wao wa lishe.

Yapo mengi Sana.

Ulishajiuliza KWANINI Simba wanapambana kujenga pale Bunju? Walisema wanatumia Hadi milioni 200 kwa ajili ya kukodi uwanja wa mazoezi tu.

Labda wewe mwenzangu mwenye akili terabaiti 10, KWAKO NYUMBA ya kupanga Ni bora kuliko kujenga ya KWAKO.

Kwako akili kubwa!
 
Kuna mtu kakata uwanja wa mazoezi?
Uwanja wa mazoezi kwani Simba hawana?

Tunachokataa ni uwanja kama huo wa wa Algeria.
 

Unavyodhani hadi timu inajenga uwanja wa namna hiyo ikose hivyo ulivyotaja.

Hata bongo bado ni muhimu ukitazama kwa muda mrefu zaidi.

Huku ikizingatia uwekezaji katika timu na kuwa inafanya vizuri.
 
Unavyodhani hadi timu inajenga uwanja wa namna hiyo ikose hivyo ulivyotaja.

Hata bongo bado ni muhimu ukitazama kwa muda mrefu zaidi.

Huku ikizingatia uwekezaji katika timu na kuwa inafanya vizuri.
Lazima wanavyo.....
Lakini why tunawapa presha kwenye jambo ambalo sio la lazima.
Na kwenye mambo ya muhimu hatuwapi presha.
Uwanja kwa hali iliyopo bongo sasa sio lazima au sio kipaumbele namba 1.
Hawana hata wataalamu wa Nutrition ila tunawapigia kelele "waalgeria wamejenga uwanja nyie mnasubiri nini"
 
Me nadhani simba na yanga wangeungana wakajenga uwanja wao wa pamoja kama wa taifa wakawa wanautumia.

Mbona Ac milan na inter wanatumia uwanja mmoja.
 
Simba ajenge uwanja angalau wa kutosha watazamaji 25,000 -30,000 tu inatosha.

Tamasha la Simba day lifanyike uwanja wa Benjamin W. Mkapa

Kikubwa wawekeze kwenye youth team na miundombinu kama gym na maboresho ya viwanja vya mazoezi.
 
Sio kwamba lazima wajenge uwanja mkuubwa wa 5ok, hapana, kibongobongo hata wa watu 25k unatosha kisha pichi nzuri nk, mechi moja tuu ndio iende taifa
 
Sio kwamba lazima wajenge uwanja mkuubwa wa 5ok, hapana, kibongobongo hata wa watu 25k unatosha kisha pichi nzuri nk, mechi moja tuu ndio iende taifa
Haina maana sasa.......
Kama unao uwanja lakini mechi zako zote kubwa unachezea Taifa.
Mfano Simba na Wydad uchezeshe kwenye watu 25k?
 
Haina maana sasa.......
Kama unao uwanja lakini mechi zako zote kubwa unachezea Taifa.
Mfano Simba na Wydad uchezeshe kwenye watu 25k?
Unaona haina faida kutokana na aina ya uchumi wetu, tickets za kima cha chini tunanunua kwa Tsh3000 ila kwa wenzetu huko ukiingiza raia 25K ni pesa ndefu sana.
 
Uwanja ni wa serikali ya Algeria kupitia kwa wizara ihusuyo michezo. Sio fedha za JS K.

Abdelaziz Bouteflike, Rais wa Algeria wa zamani ndio aliahidi kuwajengea uwanja ili wautumue baada ya kufanya vizuri Africa

Ni kama Simba au Yanga wafanye vizuri Africa halafu rais wa nchi aahidi kujenga uwanja ili timu husika iwe inautumia. Sio kuumiliki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…