Izy_Name
JF-Expert Member
- Apr 9, 2020
- 772
- 1,733
Klabu ya Simba imeingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya MobiAd kwa ajili ya kusaidia ukuzaji wa maendeleo ya soka la Vijana huku Mkataba huo ukiwa na Thamani ya 500M huku kukiwa na nafasi ya kuboresha zaidi.
“Soka la vijana ni muhimu sana. Ili uwe na timu ya vijana iliyo bora lazima iwezeshwe. Kama ilivyo kwa wachezaji wengine kama Mohamed Hussein kutoka kwa timu ya vijana.”
“Simba inakwenda mbele kutambua vipaji, kuvichukua na kuviendeleza na kuweza kutengeneza timu yenye vipaji vikubwa sana. Tunaamini Simba imara yenye vipaji haitaisaidia Simba pekee bali hata taifa letu.”
“Yawezekana wachezaji tunaowaona ni sababu ya bahati, lakini tunatengeneza mfumo ambao kila kijana mwenye kipaji tutamwezesha kukuza kipaji chake, lakini sio tu kuendeleza kipaji cha mpira lakini pia kusoma shule.”
“Leo tupo kwenye historia nyingine ya kuendeleza soka la vijana Tanzania. Mfumo wetu utakuwa mfumo wa wazi na endelevu.”
“Namshukuru meneja wa timu Patrick [Rweyemamu] sababu ametumika sana kujenga vijana ambao tunawaona leo wakifanya vizuri.”
Mtendaji Mkuu wa Simba sc Imani Kajula.
“Tumeona hii ni fursa kuungana kwenye hii safari. Tunatangaza udhamini kwa timu ya vijana ya Simba Sports Club kwa mkataba wenye thamani ya Tsh. 500 milioni kwa miaka miwili.”
“Tunaamini mpira wa miguu ni sehemu ya suluhisho la ajira kwa vijana. Simba ni timu kubwa Afrika na inazidi kuwa kubwa hivyo ni vizuri kuandaa vijana ambao watachukua nafasi ya hawa wa sasa.”
CEO wa MobiAd Africa, Rumisho Shikonyi
“Jambo hili lina neema kubwa. Niwashukuru MobiAd kwa kukubali kudhamini timu yetu ya vijana. Kama Simba SC tunawaahidi kwamba fedha hizi zitatumika vizuri kwani vijana ndio msingi wa timu yetu.”
“Tuna malengo ya kuboresha soka la vijana, shamba ambalo tunajua litatusaidia kuvuna vipaji kwa ajili ya timu ya wakubwa. Ndugu Dewji amekubali kusaidia kuendeleza soka la vijana. Hivi karibuni tutaanza ujenzi wa kituo chetu."
Mwenyekiti wa Bodi Simba sc Salim Abdallah “Try again”
Mdhamini mpya wa @simbayouthtz MobiAd Africa atakaa kifuani mwa jezi ambazo timu hiyo ya vijana itakuwa inatumia kwa kuwa ndiyo mdhamini mkuu wa klabu hiyo kwa timu za vijana.