Klabu ya Simba yatakiwa kuheshimu na kuacha kubagua vyombo vya habari

Joined
Apr 9, 2022
Posts
66
Reaction score
32
Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba kimelalamikiwa kwa kitendo chake cha ubaguzi na kutoa kauli chafu dhidi ya wanahabari kitendo kilitafsiriwa kuwa ni ukandamizaji wa tasnia ya habari.

Hayo yamejili jana katika uwanja wa Benjamini Mkapa, lilipokuwa likiendeshwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya kuingilia kwenye Tamasha la Simba day.

Wakizungumza na Mwakilishi wa Jamii Forum wamesema kuwa wamesikitishwa sana na Chiko kwa kitendo cha kutotuthamini sisi wanahabari, ebu angalia wanavyotuchukulia kama sijui kitu gani, alionekana akilalamika mmoja wa Wanahabari uwanjani hapo.

"Nimeripoti habari za Simba kwa miaka kumi sasa leo najibiwa kama mbwa mimi, nisiye na thamani, tumekuwa pamoja muda wa miezi sasa wakituita tunakuja bila hata malipo yoyote hata kutupa nauri tu hakuna lakn kwa kuwa ni wajibu wetu sisi hilo hatujali eti leo tuna ambiwa wanaopewa ni wale wanaowafahamu wao kama hakufahu hawezi kukupa tafuta utaratibu wa kuingia ndani" alisema mwandishi x.

Aliendelea kwa kusema kuwa sisi wengine kwa sababu yakuandika mazuri kuhusu Simba imepelekea kuzuiliwa kuingia kwenye shughuli za Yanga, lakini hilo hatujali ila hili la leo Simba mmetuvua nguo.

"Ebu tamaza wanahabari wanavyodhalilishwa hapo wanapangishwa foleni kama wanahesabu namba, wakati wengine wamewahita vyumbani wakawapatia hivyo vitambulisho, ambao hata kwenye shughuli nyi gi za Simba hawaonekani na sisi tupo kila shughuli yao lakni wanatufanyia hivi" alisema x

Pia wameuomba uongozi wa Simba kutokuruhusu vitendo kama hivyo kwa kuwa vinaleta picha mbaya kwa klabu hiyo.

Simba ni klabu kubwa Tanzania na nje ya Tanzania hivyo basi ikiruhusu tena makosa kama haya dhidi ya wanahabari itaondoa ile taswira imara mbale ya jamii.
 
Sawa watajirekebisha.wameghafirika nice binadamu.
Msiache kuisema Simba vizuri ndo timu kubwa hapa Tanzania .ila wale utopolo wasemeni mpaka wapoteane
 
Hivi vyombo vya habari vimekuwa vingi vidogo vidogo halafu ni hizi YouTube channel waandishi hawana uweledi na kuna baadhi wamevamia tu bila taaluma ili kurun tv channel YouTube.

Kuna clip moja Bumbuli anahojiwa akamwambia ripota siku nyingine msinifuate mnaweka tu meza hamna ofisi halafu barabarani ,kuweni na ofisi za kueleweka nitakuja.

Mtu hajajiandaa , hana taarifa ,taasisi anayofanyia kazi haina taarifa ,hajui anaulizwa nini kasimamisha tu gari wamemwona analetewa meza mbovu.

Siwalaumu Simba lazima siyo kila chombo cha habari kuruhusiwa, hamna ofisi ya maana ,camera ya maana baadaye mnaonekana wote wa hovyo, hamna anayeweza kukataa chombo kinachoelewa na kinajulikana.
 
Huyo kanjanja alitaka akiitwa na Simba SC apewe na nauli ndio maana amekasirika, hawa waandishi njaa ndio wanawekwa mfukoni siku hizi na yule muarabu wanaanza kumpamba asubuhi mpaka usiku.

Anataka awe anapewa bahasha Simba then akitoka hapo akapewe na muarabu, huu ujinga wao ndio unawafanya wadharaulike, iko siku wataumbuliwa vibaya sana.
 
Hivi Wanahabari ( Waandishi wa Habari ) huwa wanatakiwa wakiitwa mahala Kuchukua Habari walipwe chochote Kitu na wapewe Nauli?

Je, Maadili yao ya Kazi hivi ndivyo huwa yanawataka Kufanya au Kufanyiwa? Kama nawe ni Mwenzao ( Journalist ) na Unaliunga hili Mkono basi ninaanza Kukudharau na hata Kukuona ni 'Nut' pia.

Kwa jinsi Waandishi wa Habari wengi wa sasa mlivyo ( walivyo ) Wanafiki huku 75% wakiwa katika Payroll ya Yanga SC ( hasa Mdhamini Mkuu GSM ) naunga mkono Uongozi wa Simba SC Kuwafanyia / Kuwafanyieni hiki ( hicho ) walichowafanyieni na tena GENTAMYCINE natamani wawapigeni hata Vibao ( Kelebu ) kabisa Ili Mkome na Mbadilike.

Wapuuzi wakubwa nyie....!!!!
 
Hili sasa siyo soka tena bali soko.
Imekuwa vita siyo utani tena
 
Hivi vyombo vya habari vimekuwa vingi vidogo vidogo halafu ni hizi YouTube channel waandishi hawana uweledi na kuna baadhi wamevamia tu bila taaluma ili kurun tv channel YouTube.

Kuna clip moja Bumbuli anahojiwa akamwambia ripota siku nyingine msinifuate mnaweka tu meza hamna ofisi halafu barabarani ,kuweni na ofisi za kueleweka nitakuja.

Mtu hajajiandaa , hana taarifa ,taasisi anayofanyia kazi haina taarifa ,hajui anaulizwa nini kasimamisha tu gari wamemwona analetewa meza mbovu.

Siwalaumu Simba lazima siyo kila chombo cha habari kuruhusiwa, hamna ofisi ya maana ,camera ya maana baadaye mnaonekana wote wa hovyo, hamna anayeweza kukataa chombo kinachoelewa na kinajulikana.
Naungana na wewe binafsi sizipendi vyombo vya habari vya youtube uweza kukuta Wana hii tabia ya kuweka kichwa Cha habari hayashabiani na maudhui yaliyozungumzwa kwenye interview
 
Acha kulalamika lalamika bro,mbona hakuna baya hapo,msingepanga mistari wa kwanza kuja angekua wa mwisho kuondoka je ingekua sawa?
 
View attachment 2317520Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba kimelalamikiwa kwa kitendo chake cha ubaguzi na kutoa kauli chafu dhidi ya wanahabari kitendo kilitafsiriwa kuwa ni ukandamizaji wa tasnia ya habari.View attachment 2317521
Hayo yamejili jana katika uwanja wa Benjamini Mkapa, lilipokuwa likiendeshwa zoezi la utoaji wa vitambulisho vya kuingilia kwenye Tamasha la Simba day.

Wakizungumza na Mwakilishi wa Jamii Forum wamesema kuwa wamesikitishwa sana na Chiko kwa kitendo cha kutotuthamini sisi wanahabari, ebu angalia wanavyotuchukulia kama sijui kitu gani, alionekana akilalamika mmoja wa Wanahabari uwanjani hapo.View attachment 2317523

"Nimeripoti habari za Simba kwa miaka kumi sasa leo najibiwa kama mbwa mimi, nisiye na thamani, tumekuwa pamoja muda wa miezi sasa wakituita tunakuja bila hata malipo yoyote hata kutupa nauri tu hakuna lakn kwa kuwa ni wajibu wetu sisi hilo hatujali eti leo tuna ambiwa wanaopewa ni wale wanaowafahamu wao kama hakufahu hawezi kukupa tafuta utaratibu wa kuingia ndani" alisema mwandishi x.View attachment 2317524

Aliendelea kwa kusema kuwa sisi wengine kwa sababu yakuandika mazuri kuhusu Simba imepelekea kuzuiliwa kuingia kwenye shughuli za Yanga, lakini hilo hatujali ila hili la leo Simba mmetuvua nguo.

"Ebu tamaza wanahabari wanavyodhalilishwa hapo wanapangishwa foleni kama wanahesabu namba, wakati wengine wamewahita vyumbani wakawapatia hivyo vitambulisho, ambao hata kwenye shughuli nyi gi za Simba hawaonekani na sisi tupo kila shughuli yao lakni wanatufanyia hivi" alisema x

Pia wameuomba uongozi wa Simba kutokuruhusu vitendo kama hivyo kwa kuwa vinaleta picha mbaya kwa klabu hiyo.

Simba ni klabu kubwa Tanzania na nje ya Tanzania hivyo basi ikiruhusu tena makosa kama haya dhidi ya wanahabari itaondoa ile taswira imara mbale ya jamii.

Huyo mwandishi X kama anashindwa kuandika ‘Nauli’ anawezaje kuandika hizo habari anazosema za Simba kwa miaka 10?
 
Kwa style hii ya uandishi wa kulalamika qcha unyimwe tu ticket.
 
Back
Top Bottom