Klabu ya Simba yatoa Ratiba ya mkutano mkuu wa kawaida kwa mwaka 2026

Klabu ya Simba yatoa Ratiba ya mkutano mkuu wa kawaida kwa mwaka 2026

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba imetangaza ratiba ya uchaguzi wa viongozi pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka 2026, kwa mujibu wa Katiba ya klabu hiyo ya mwaka 2018 (Toleo la 2026).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 26, 2026, uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo utafanyika Januari 3, 2027, jijini Dar es Salaam.

Aidha, Bodi imeeleza kuwa taarifa kuhusu vikao na ajenda nyingine za mkutano huo zitatolewa kwa wanachama kupitia matawi yao. Wanachama wote wa Simba wamehimizwa kushiriki katika mkutano huo muhimu kwa mustakabali wa klabu.

Taarifa hiyo imetolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, ikieleza utaratibu wa maandalizi ya mkutano na uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2027.

Chanzo: Simba Instagram page

simba.jpeg
​
 
Back
Top Bottom