Klabu ya Valencia CF yamuenzi shabiki wake kipofu kwa sanamu uwanjani

Klabu ya Valencia CF yamuenzi shabiki wake kipofu kwa sanamu uwanjani

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Valencia.jpg

Hakika bila mashabiki, mchezo wa mpira wa miguu si kitu!

Timu ya Valencia imeweka sanamu katika kiti cha shabiki wake (sasa ni marehemu) ambaye alihudhuria uwanjani hapo kutazama kila mchezo hata baada ya kupofuka.

Timu hiyo imeweka sanamu ya kumuenzi Vicente Navarro Aparicio, aliyekuwa shabiki kindakindaki wa Valencia, ambaye pia alikuwa mwanachama Namba 18 wa timu hiyo.

Vicente alitazama kila mchezo wa nyumbani kwenye uwanja wa klabu hiyo wa Mestalla, na alisafiri kwenda kuishabikia timu yake kwenye mechi za ugenini. Vicente pia aliyashuhudia mashindano ya Copa del Generalísimo ya mwaka 1967 (sasa inayojulikana kama Copa del Rey) ambapo timu yake ilipata ushindi dhidi ya Athletic Bilbao.

Vicente alipoteza uwezo wa kuona alipokuwa na umri wa miaka 54 na kumsababisha kushindwa kutazama mechi za timu yake aliyoipenda sana.

Hata hivyo, upofu haukumzuia kuendelea kuhudhuria uwanjani, na alikuwa akifanya hivyo na mwanaye wa kiume. Vicente alitaka kuhisi mazingira ya uwanjani wakati akifuatilia matukio kwa ufafanuzi anaopewa awapo uwanjani hapo.

Shabiki huyo pia likuwa uwanjani hapo kwa msimu wa mwaka 2004 ambapo timu yake iliibuka mshindi mara mbili, akielezea kuwa huo ulikuwa mwaka wa furaha zaidi katika maisha yake.

Vicente aliaga dunia miaka miwili iliyopita lakini Valencia wamemuenzi kwa kuweka sanamu yake katika kiti chake, hivyo ataendelea kuwepo katika mechi za Valencia milele!

===========

Valencia put statue in seat of late fan who watched every game even after turning blind

What is football without fans? Nothing.

Fans are the lifeblood of the game and the story of a late Valencia season ticket holder proves just how much it means to some.

Vicente Navarro Aparicio was an avid Valencia supporter. He was Valencia CF member No.18 and watched every home game at the club’s Mestalla stadium.

Vicente also travelled to away games, witnessing the 1967 Copa del Generalísimo - now known as the Copa del Rey - final win over Athletic Bilbao.

But Vicente lost his sight at the age of 54 due to a detached retina.

Sadly, Vicente was unable to watch his favourite team. But his support for Valencia never waned.

Statue honours Vicente at Mestalla

He kept on coming to Mestalla with his son. Vicente wanted to feel the atmosphere and he would follow along by having the events on the field described to him.

Vicente was present for the 2004 double-winning season, describing it as the happiest year of his life.

He passed away two years ago but Valencia have honoured him by putting a statue of him in his seat.

His bronze figure sits in seat 164 of row 15 in the Tribuna Central section.

The story has been told in a wonderful video, which features Vicente’s son discussing his father’s love of football.

Simply incredible.

Now, Vicente will forever be at Valencia games.

Modern technology has paved the way for more blind fans to still enjoy attending football matches.

Liverpool supporter Ian Wood, who has been blind since the age of five, watches the Reds play using a £600 vision helmet.

The helmet works by enhancing the images from a high-definition camera and playing them on a screen held over Ian’s eyes.

“This has changed my life. I've been a fan since I was a boy and remember going to a match in the 1990s and they didn't even have audio-commentary, so this is amazing," he told the Mirror.

"After years of listening from the sidelines, I can actually shout to the ref 'that was never a penalty' if I don't like what I see.

"I can't read the names on players' shirts, but I can tell who has the ball. I get so much more from the game than I did before."


Source: GIVEMESPORT
 
Back
Top Bottom