Klabu ya Yanga Sc imemrejesha Ali Shaban Kamwe kwenye nafasi yake ya Umeneja wa Habari na Mawasiliano na Tayari amesaini Mkataba Mpya wa miaka miwili

Klabu ya Yanga Sc imemrejesha Ali Shaban Kamwe kwenye nafasi yake ya Umeneja wa Habari na Mawasiliano na Tayari amesaini Mkataba Mpya wa miaka miwili

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Klabu ya Yanga Sc imemrejesha Ali Shaban Kamwe kwenye nafasi yake ya Umeneja wa Habari na Mawasiliano na Tayari amesaini Mkataba Mpya wa miaka miwili ndani ya Klabu hiyo.

Uamuzi huo wa kumrejesha umefanywa na Rais wa Yanga Eng. Hersi na Makamu wake Arafat Haji baada ya Kamwe kueleza changamoto zake kwa viongozi zilizompelekea kuchukua uamuzi huo kwa maslahi ya pande zote mbili na wamekubaliana kuzifanyia kazi.

#KitengeSports
 
Bora, haiwezekani jitu lililowaita hamna akili, yaani yanga woote, wenye akili ni sunday manara na mzee kikwete halafu leo mmpe kazi hapo ingethibitisha upunguwani,
Hongereni wazee wa utopolo, huyu mnafiki mpigeni kibuti ikiwezekana abaki shabiki au mwanachana tu kama akitaka.
 
sikutegemea koment kama hii kutoka kwako.
Mnawakuza hao wasemaji, ajira zao hazitakiwi kuwa tofauti na za mhasibu au mfagizi? Eti mkataba wa miaka miwili? Ndiyo maana kina Haji wanajiona wako level za CEO, wanajitapa wana endorsements kuzidi hata wachezaji, we umeona wapi kitu kama hicho kwa mwajiriwa wa klabu ya mpira?
 
duuu..sasa mtu kakuzwa kwa kupewa mkataba wa miaka miwili?
 
Mimi ni mpenzi wa mpira tena mpenzi wa Klabu pendwa ya Wananchi. Nimesikitishwa sana na taarifa ya Ali Kamwe kutangaza kujiuzulu kuwa msemaji wa Klabu ya Wananchi.

Ninamshauri Rais wa Yanga, Eng. Hersi kufanya kila njia kuhakikisha Ali Kamwe anaendelea na majukumu yake katika Klabu ya Yanga.

Huyo kijana kusema kweli amei brand Klabu ya Yanga na hakuna aliyefanya kazi nzuri kama Ali Kamwe. Manara akirudi Yanga nashauri apewe majukumu mengine. Ali Kamwe ni kipenzi cha mashabiki na hatutaki kumpoteza.
 
unalala sana mkuu...
 
Pamoja na kwamba umepitwa na current updates za habari hii, ila ninachoweza kuobserve ni kwamba huyu kijana alitaka labda ashinikize uongozi umpe mkataba mpya ili awe na uhakika na maisha, na alifanya hadharani ili uongozi upate shinikizo la mashabiki kurenew mkataba. Katika hali ya kawaida, angeweza tu kuongea na uongozi bila watu wa nje ya uongozi kujua, maana wengi tu naamini tulikuwa wala hatuna hata habari kuwa mkataba wake unaisha
 
Mkuu ali kamwe amechukuliwa na simba....kaenda kuwa kocha wa viungo🤣🤣🤣🤣🤣
 
Baada ya kukikali kitu cha usemaji kwa takribani miaka miwili hatimaye, Ali kamwe apokonywa tonge.

Ni Haji Manara baada ya kifungo chake kutamatika hatimaye amerudi kwenye kiti chake, huku bwana mdogo akiugulia maumivu kwa ndani. Waswahili wanasema usiache mbachao kwa msala upitao. Pole sana kamwe. Ukileta fyoko Manara anakutia makwenzi, na inasemekana kamwe ni mbishi akiambiwa aende dubai na boss yeye hukataa, lakini Manara yeye hanaga shida.

3A97D0D9-CE33-4D7E-BEB2-7BB610327EB1.jpeg
 
Mbona nimesikia karudishwa kwenye nafasi yake
 
Back
Top Bottom