Klabu ya Yanga yatangaza rasmi kuwatema wachezaji Yacouba na Chiko

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Uongozi wa klabu ya Yanga leo Julai 19,2022 imetangaza rasmi kuwatema wachezaji Yacouba Sogne na Chiko Ushindi ili kubaki na wachezaji 12 wa kigeni.

"Wengi mtajiuliza kwanini tuna wachezaji 14 na kanuni zinataka wachezaji 12 tu, wachezaji wetu ambao hatutakuwa nao kwa msimu ujao kwa wachezaji wa kigeni ni Chiko Ushindi na Yacouba Sogne baada ya makubaliano ya pande zote mbili".

"Tunaachana na Chiko Ushindi ambaye tuliingia naye makubaliano maalumu akitokea Tp Mazembe na tutafanya mazungumzo ya kuachana pia na Yacouba Sogne, ambaye hayupo fiti kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwasababu ya kusumbuliwa na majeruhi". Msemaji wa Yanga Haji Manara.

Wakati huo huo Yanga wameamua kuweka Kambi Kigamboni Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/2023, Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.

Msemaji wa Yanga Haji Manara akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali kutoka klabu ya Yanga SC.
 
Yacouba Sogne kiherehere cha kuvaa Jezi ya Aziz Ki na kupita huku na kule kimemuisha kabisa yaani.

Si ndio nyinyi mliokuwa mkisema kwamba AZIZ KI Ametoa amri kuwa Rafiki yake ni “lazima” abaki?

 
1) Diarra
2) Bangala
3) Aucho
4) Chico
5) Makambo
6) Mayele
7) Moloko
8) Morrison
9) Kambole
10 Birigimana
11) Aziz k
12 Djuma Shaban

Wa 14 wakina nani au wanasajili wengine?
 
Yacouba Sogne kiherehere cha kuvaa Jezi ya Aziz Ki na kupita huku na kule kimemuisha kabisa yaani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] atajutraaaaaa,
 
Si ndio nyinyi mliokuwa mkisema kwamba AZIZ KI Ametoa amri kuwa Rafiki yake ni “lazima” abaki?
View attachment 2296509
Sasa imekuwaje tena Meneja Ushawishi kuachwa? Kazi yote aliyoifanya

Halafu si huwa wanasema Yanga hawezi kuacha mchezaji kwa sababu ya majeruhi, Kauli hii imesahaulika mara hii.
 
Ni maamuzi sahihi kabisa. Na hakukuwa na namna nyingine ya kuwasaidia, isipokuwa kuwaruhusu tu ili wakatafute changamoto mpya mahali pengine.
 
Sasa imekuwaje tena Meneja Ushawishi kuachwa? Kazi yote aliyoifanya..
Usikariri maisha Mkurugenzi. Ameachwa Mapinduzi Balama, mchezaji mwenye kipaji cha hali juu kabisa nchini na aliyewanyoosha kwenye ile mechi ya sare ya 2-2! Halafu unaongea nini!!
 
Usikariri maisha Mkurugenzi. Ameachwa Mapinduzi Balama, mchezaji mwenye kipaji cha hali juu kabisa nchini na aliyewanyoosha kwenye ile mechi ya sare ya 2-2! Halafu unaongea nini!!
Muwe mnajifunza kuweka akiba ya maneno sasa, na si kuropoka tu

Simba SC ilitaka kumuacha Taddeo Lwanga kwasababu ya majeruhi ya muda mrefu.

Mlipiga kelele sana nyie kuwa hii si haki, bila kujua hizi klabu zinaendeshwa kwa malengo.
 
Yacouba Sogne kiherehere cha kuvaa Jezi ya Aziz Ki na kupita huku na kule kimemuisha kabisa yaani.

Kwa maamuzi haya ya klabu, yamkini hatakaa aje asahau.
Unapost na unacoment we mwenyewe, ulitaka avae jezi ya john boko au Mzamiru yassini?
 
Unapost na unacoment we mwenyewe, ulitaka avae jezi ya john boko au Mzamiru yassini?
Mbona hakuna la ajabu hapo mtani?

Uzi ni kama mdau wa Kabumbu la Ligi Kuu na viwango vya CAF

Uchangaaji ni kama shabiki na mwanachama hai wa Mnyama Mkali Mwituni.

Hakuna Sheria inayomzuia mtoa mada kutochangia hiyo mada kwa maoni yake.
 
1) Diarra
2) Bangala
3) Aucho
4) Chico
5) Makambo
6) Mayele
7) Moloko
8) Morrison
9) Kambole
10 Birigimana
11) Aziz k
12 Djuma Shaban

Wa 14 wakina nani au wanasajili wengine?
Kwa mujibu wa taarifa ambazo wamezitangaza wao wenyewe hii leo

Je.? Yacouba na Joyce wapo hapo kwenye kikosi chako.
 
Yacouba alikua anampambania Aziz kwioo kumbe yeye ndo anampisha[emoji23][emoji23][emoji23]
Wachezaji wanatambua kwao mpira ni ajira! Hivyo Yacouba Sogne kuondoka Yanga, kwake siyo big deal kama unavyo chukulia wewe.

Muhimu tu wamalizane kwa kufuata taratibu na makubaliano ya mkataba wao.
 
Wewe utakuwa unachanganya madesa! Yaani sisi mashabiki wa Yanga tupige kelele kwa sababu ya kuachwa mchezaji wenu!

Zitakuwa ni kelele za kuwachora tu bila shaka.
Kuchanganya kwa wapi, hapa walikuwa wakijinasibu kuwa angalia Balama Mapinduzi amepelekwa Afrika Kusini kupata matibabu, na kulaumu Simba kuwa inakuwaje aachwe mchezaji akiwa majeruhi.

Zilikuwa ni huruma ama tambo..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…