Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Uongozi wa klabu ya Yanga leo Julai 19,2022 imetangaza rasmi kuwatema wachezaji Yacouba Sogne na Chiko Ushindi ili kubaki na wachezaji 12 wa kigeni.
"Wengi mtajiuliza kwanini tuna wachezaji 14 na kanuni zinataka wachezaji 12 tu, wachezaji wetu ambao hatutakuwa nao kwa msimu ujao kwa wachezaji wa kigeni ni Chiko Ushindi na Yacouba Sogne baada ya makubaliano ya pande zote mbili".
"Tunaachana na Chiko Ushindi ambaye tuliingia naye makubaliano maalumu akitokea Tp Mazembe na tutafanya mazungumzo ya kuachana pia na Yacouba Sogne, ambaye hayupo fiti kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwasababu ya kusumbuliwa na majeruhi". Msemaji wa Yanga Haji Manara.
Wakati huo huo Yanga wameamua kuweka Kambi Kigamboni Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/2023, Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.
Msemaji wa Yanga Haji Manara akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali kutoka klabu ya Yanga SC.