Klabu zilizokusanya alama nyingi CAF msimu huu 2022/2023

room

Member
Joined
Dec 28, 2015
Posts
61
Reaction score
102
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) hivi karibuni limetoa orosha ya vilabu vinavyoongoza kwa ubora barani humo kwa mwaka 2023.

Watani wa jadi nchini Tanzania Simba na Yanga wameonekana kuongeza alama huku kila mmoja akipanda katika viwango vya ubora CAF.

Simba ambayo ilikuwa nafasi ya 11 msimu uliopita, imepanda mpaka nafasi ya 9 huku Yanga ikitoka nafasi ya 78 mpaka nafasi ya 18 Barani Afrika, hii inatokana na alama ambazo kila klabu imekusanaya kwa misimu mitano mfululizo.

Timu zilizokusanya points nyingi zaidi kwenye michuano ya CAF 22/23.

1. Alama 30 — Al Ahly

2. Alama 25 — Wydad Casablanca

2. Alama 25 — USM Alger

3. Alama 20 — Young Africans

4. Alama 20 — Mamelodi Sundowns

5. Alama 20 — Esperance.

◉ Muda kama huu msimu uliopita Young Africans SC walikuwa wa (78) kwenye viwango vya CAF wakiwa na points 0.5.

◉ Baada ya msimu (1) Yanga wanesogea kutoka nafasi ya (78) hadi (18) wakiwa na points (20). Klabu ya Simba SC imesogea kutoka nafasi ya (10) hadi (9) wakiwa na jumla ya points (35). Anayeongoza Al Ahly yeye ana jumla ya points (83).

Viwango vya (CAF) hupangwa kwa kuzingatia performance ya timu husika ndani ya misimu (5) kwenye michuano ya (CAF).

◉ Simba SC wamekusanya points (35) katika misimu hiyo (5) na kukaa nafasi ya (9). Huku Yanga wakikusanya points (20) katika msimu (1) 22/23 pekee na kukaa nafasi ya (18).

Misimu (4) iliyopita Young Africans hawakufanya vizuri kwenye michuano ya CAF, hawakupata points that's why wanabaki na points (20) walizozikusanya 22/23.

◉ Baada ya kupata points (20) 22/23, kwa mara ya kwanza Young Africans wamezipita klabu zifuatazo kwenye viwango vya CAF.

ASEC Mimosas

Etoile du Sahel

ES Setif

Coton Sports

Marumo Gallants

Kaizer Chiefs

AS Vita

Al Merriekh

Al Masry

US Monastir

FAR RABAT

Enyimba

MS Alger.
 
Kusema kuwa Yanga wamefika nafasi hiyo kwa msimu mmoja tu siyo sahihi wakati unakiri mwenyewe kuwa CAF wanaweka hiyo ranking kwa kuangalia miaka 5. Hata kama miaka 4 ya nyuma Yanga haikupata points ila bado imeangaliwa.
 
Hiyo ni ranking kwa msimu mmoja tu wa 2022/2023 pekee.
Award point kwa klabu bingwa
Bingwa anapata point 6
Mshindi wa pili point 5
Wanaoishia nusu point 4
Wanaoishia robo point 3
Wanashika nafasi ya tatu kwenye kundi point 2
Wanaoshika nafasi ya mwisho kwenye kundi point 1

Upande wa shirikisho CAF

Bingwa anapewa point 5
Mshindi wa pili point 4
Nusu fainali point 3
Robo fainali point 2
Wa tatu kwenye kundi point 1
Wa mwisho point 0.5

Hizo point zinazidishwa na coefficient ya msimu husika ndipo unapata jumla ya point. Hivyo mleta mada yupo sahihi kwa msimu wa mwaka ulioisha kwa kitendo cha Yanga kucheza fainali kavuna point 20 ( 4x5) na kitendo cha Al Ahly kuchukua kombe kavuna alama 30 (6x5) kama utachukulia kwa 5 year ranking Al Ahly wana point 83
 
Yaani ilimradi ubishe tu umekiri kwamba miaka 4 hawakukusanya points zozote hizo walizo pata wamekusanya kwa msimu mmoja sasa unacho ongea ni nini

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Maelezo yote ya nini hapo wakati hoja ni kuwa CAF wanaangalia misimu mitano ambayo hata yeye amesema. Sasa utasemaje tena kuwa Yanga amefika hapo kwa msimu mmoja kisa hawakuambulia points kwa misimu iliyopita. Ni sawa mnavyojitapa kuwa Simba wamehangaika kila msimu wanaishia robo halafu Yanga msimu mmoja tu imefika fainali, kwani Yanga miaka yote ilikuwa haishiriki mashindano ya CAF?

Jaribu kuboresha uwezo wako wa kuelewa maandiko unayosoma.
 
Nikuulize swali dogo tu, kabla ya msimu wa 2022/2023 Yanga walikuwa na point ngapi katika CAF ranking?
 
Point ni kuwa CAF wanaangalia misimu mitano kama alivyosema mleta mada, hayo mengine ni porojo tu. We itakuwa shule umekula sana fimbo
 
Kusema kuwa Yanga wamefika nafasi hiyo kwa msimu mmoja tu siyo sahihi wakati unakiri mwenyewe kuwa CAF wanaweka hiyo ranking kwa kuangalia miaka 5. Hata kama miaka 4 ya nyuma Yanga haikupata points ila bado imeangaliwa.
Rudi shule dogo
 
Point ni kuwa CAF wanaangalia misimu mitano kama alivyosema mleta mada, hayo mengine ni porojo tu. We itakuwa shule umekula sana fimbo
Ulichoulizwa na ulichokijibu ni tofauti. Nimekuuliza kabla ya msimu wa 2022/2023 nitajie point za Yanga zilikuwa ni ngapi? Utajua mwenyewe kama utakusanya ya miaka minne au mingapi ila nataka uniambie misimu ya nyuma yake Yanga ilikuwa na point ngapi
 
Maelezo yote ya nini hapo wakati hoja ni kuwa CAF wanaangalia misimu mitano ambayo hata yeye amesema. Sasa utasemaje tena kuwa Yanga amefika hapo kwa msimu mmoja kisa hawakuambulia points kwa misimu iliyopita. Ni sawa mnavyojitapa kuwa Simba wamehangaika kila msimu wanaishia robo halafu Yanga msimu mmoja tu imefika fainali, kwani Yanga miaka yote ilikuwa haishiriki mashindano ya CAF?

Jaribu kuboresha uwezo wako wa kuelewa maandiko unayosoma.
We MBUMBUMBU ni hivi,katika mikaa mitano minne yote hakupata point yoyote na mwaka huu mmoja tu ndo amepata mkupuo wa point 20 na ndo zimemsogeza mpaka hapo alipo.
 
Yaani ilimradi ubishe tu umekiri kwamba miaka 4 hawakukusanya points zozote hizo walizo pata wamekusanya kwa msimu mmoja sasa unacho ongea ni nini

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
kuna tofauti Kati ya 0 na - , 0 ni alama (marks) kwa mshiriki ila - ni kwamba hakukua na ushiriki. Nikupe mfano wa darasani 0 ni mwanafunzi kafanya mtihani na hicho ndicho kaambulia, kwenye majumuisho yake inajumlishwa kupata jumla na wastani maana ni alama aliyopata. - Manake mwanafunzi hakufanya mtihani.

Kama Yanga alishiriki kimataifa katika hiyo miaka mitano basi aliambulia kitu ambacho ni 0 na kinajumlishwa pia, 0 ina beba maana yake na - inabeba maana yake
 
Back
Top Bottom