KLM waomba radhi kufuatia kuchapisha taarifa ya kuwa kuna Civil Unrest Nchini Tanzania

KLM waomba radhi kufuatia kuchapisha taarifa ya kuwa kuna Civil Unrest Nchini Tanzania

James Hadley

Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
36
Reaction score
29
FB_IMG_1675007191983.jpg
 
Wapuuzi Hawa walitumika ili kuua utalii wa nchi yetu
Ukoloni mpya unarudi katika njia mbalimbali; hii ni mojawapo.
Hawa wazungu wanahangaika sana siku hizi, hasa wanapoona njia zao za kuwatawala wengine zinaendelea kufifia. Wanatapatapa sana siku hizi.
 
Nitaiamini vipi hii taarifa ya wakosefu kuombewa msamaha tena na serikali yetu?!

Ila kama ni kweli, aisee tuna safari ndefu sana!.
Aiiiseeee!

Imenibidi nikusome mara mbilimbili ili nipate uzito kamili wa hii mistari miwili uliyoandika hapa!

Lingekuwa jambo tofauti kabisa kama Wizara wangeonyesha angalau kisehemu tu cha "kuomba msamaha" kikiambatana na barua hii ya Wizara.

Kuonyesha kwamba KLM hawakuomba msamaha (kwa dhati); jamaa bado wamekomalia hadi hiyo Jan. 30!
Yaani bado wanashiriki katika mambo ambayo wameyaombea msamaha?

Sielewi ni kitu gani kinamsibu Profesa wetu huyu, kwa maana hapo zamani nilimpa heshima sana.
 
Leteni hiyo apology statement!

Hivi nikikukosea, wewe ndio unawaambia watu nimeomba radhi au mimi ndio naomba radhi kisha wewe ikufikie?

Nahisi sielewi kitu hapa….
Tuliwapiga klm mkwara ili waombe radhi lakini wakameza jiwe. Sasa tumeona tuandike sisi kwamba wao wanetuomba msamaha, halafu tuone kama wana jeuri ya kukanusha.
Halafu na wewe kuwa mzalendo. Hiyo barua ya apology unaitaka ya nini?
 
• "Following the ministrys' statement..."
• "its flights to Zanzibar has resumed with an immediate effect..."
• "the" zimekuwa nyingi sana, sijui hakufundishwa matumizi ya articles 🙄

Kingereza cha wapi hiki?

Shame on him and the ministry!
 
Ukoloni mpya unarudi katika njia mbalimbali; hii ni mojawapo.
Hawa wazungu wanahangaika sana siku hizi, hasa wanapoona njia zao za kuwatawala wengine zinaendelea kufifia. Wanatapatapa sana siku hizi.

21Century bado unawaza mambo ya ukoloni???
Change ur mind
 
Mbona Kama taarifa ya US embassy na KLM vinafuatana hizi issue zimekaa kimchongo
 
Kiukweli sijafurahishwa na hii taarifa ya wizara. Kiutaratibu ilitakiwa KLM ndo watoe statement ya kuomba msamaha na sio wizara waje na kauli kwamba KLM waliomba msamaha faragha. KLM wameikosea Tanzania na sio wizara na viongozi wake. Hii statement ya leo ni kama sisi ndo tumewaomba msamaha KLM.
 
Back
Top Bottom