KMC FC yadhulumiwa Penati: Sasa mechi zote tunataka refa toka nje ya nchi

KMC FC yadhulumiwa Penati: Sasa mechi zote tunataka refa toka nje ya nchi

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Katika mchezo wa KMC dhidi ya Yanga, Shedrack Boka alifanya faulu ya wazi na ni penalty lakini kwakuwa refa kwa sababu alizo nazo pekee na woga kwa mashbiki wa Yanga akaamua kufunika na kusababisha KMC kukosa pointi moja na imewaadhiri sana.

Kuanzia msimu ujao tunaomba Mechi zote tutumie marefa toka nje ya nchi, hawa wa ndani wabaki UMISHUMTA na UMISETTA.

Kulikuwa Red CArd Yanga tulipaswa kupewa lakini Refa wa Tanganyika akafunika, hizi timu ndogo hazotkaa zifike pahala.

Mwamuzi alikuja akiwa anaenda kutoa kadi njano, akafika wakati Okello anamshinikiza atoe kadi ya njano na from there mwamuzi akakosa confidence na akaharibu mchezo mzima.

Waamuzi wetu kwenye kutaka ku-balance mambo ndipo wana haribu, kwenye mechi nzima Yanga hatukuwa bora, kwakuwa tulikuwa na uchovu kukipiga na Simba lakini kwakweli waamuzi wanapendelea sana Big three yaani Azam, Simba na Yanga.
 
Back
Top Bottom