Kobe Bryant na mwanaye Gianna wazikwa

Kobe Bryant na mwanaye Gianna wazikwa

Nilienda Immigration kuomba passport wakaniambia nilete ushahidi wa safari nkawambia naenda kushiriki maziko ya Kobe Bryant sasa kama wamezika kimya kimya si ntanyimwa pass wakuu
 
Mmmh,mbona mkuu niliona YouTube ile helcopter inawaka moto kabisa na ikateketea?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana nandio maana week ilioisha kama ulifuatilia walichunguza wakasema itachukua miezi 17 kama sikosei kujua nn kilikuwa chanzo cha ajali hiyo bado wanaendelea kuchunguza mpaka hiyo mienzi itakapoisha watakuja na jibu kamili.
 
Kweli Mkuu! Hebu fikiria wale walokuwa wanabishana namna ya kumzika Mzee Mugabe wamepata nini?
Mazishi yanatakiwa hivi ,sio kusumbua watu,

Wazungu hata huko america , maiti inazikwaga hata na watu watatu ,


Watu waendelee na shughuli nyingine , Sio kuzungusha maiti mwezi mzima , hizi mambo utazikuta Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mazishi yanatakiwa hivi ,sio kusumbua watu,

Wazungu hata huko america , maiti inazikwaga hata na watu watatu ,


Watu waendelee na shughuli nyingine , Sio kuzungusha maiti mwezi mzima , hizi mambo utazikuta Africa
Kuna Mzee mmoja jirani yangu, Mr. Kelly.

Mzee War Hero, mkazi wa New York City.

Nilimzika.

Nikishangaa sana.Alizikwa na Funeral Home.

Wakati naanza kazi Wall St. Mr. Kelly alikuwa jirani yangu.

Halafu Mr. Kelly alikuwa anajua mipigo.

Nikirudi nyumbani nimevaa siti zangu za Wall St , Mr Kelly alikuwa si mtovu wa sifa, alikuwa anasifia suti zangu za Wall St. mpaka naona noma.

Mara moja moja nilikuwa nakaa naye nje, in the heat of the summer, tunaongea.

Ananihadithia ali yopigana vita vikuu vya pili, ali yomali,a vita, alivyotembelea Australia, watoto wazuri wa ki,ungu walivyokuwa wanajigonga kwake, ali yoamua kurudi New York.

Mpaka alivyokutana nami mchizi kutika Tanzania.

Basi tukazoeana vizuri sana, yeye alifurahia sana kuona kijana mdogo mweusi anayefanya kazi Wall St. Mimi nilipenda sana kusikiliza his "War Stories".

Tatizo la Mr. Kelly, alikuwa anaishi kivyake, hakuwa na familia. Alikuwa na binti zake wanakuja kumtembelea kama mara moja au mbili kwa mwaka kutika Pennsylvania.

Sasa, kuna siku New York City kukapiga winter storm.

Mr. Kelly kama soldier mtu wa kazi, akatika nje ku clear ile snow.

Katika ku clear ike snow akawa kajipitisha uwezo wake, uwezo wa moyo wake kufanya kazi. Akapata heart attack.

Nikaambiwa na rafiki zangu majirani Mr. Kelly amefariki.

Nilihuzunika sana.

Jirani wangu mwingine akanitaarifu Funeral home schedule. Nikaenda.

Kwenye kuzika, mama wa watoto na watoto wakaishia funeral home. Kulikuwa na ki storm bado siku hiyo.

Lakini hawakumzika baba yai wale mabinti, waliishia Funeral Home tu.

Mimi na jirani yangu mmoja Mama M Jamaica tukaishia kwenda makaburini kuzika.

Nilisikitika sana.

Kwa sababu mimi niliona mtu kama yule alitakiwa kuzikwa na familia yake kubwa.

Lakini hayo ndiyo maisha.

Pengine, ndiyo maisha aliyojichagulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom