Huko nyumbani kuna kijiji kinaitwa Koboko kutokana na huyo nyoka.. Kila mara lazima usikie mazishi, chanzo ni koboko.. Nilikuaga nasikia stori zake tuu, ila sikumtilia maanani..
Siku hiyo natoka sehemu fulani nikakatiza kwenye hicho kijiji ili nitokee kijiji chetu, kuna kanjia kanakatiza msituni na mto.. Sina hili wala lile, narusha mikono huku na kule natembea kwa raha zangu..
Hamadi!! Mita kama 4-5 toka nilipokuwepo nikamuona koboko rangi ya kijivu na weusi katanda njiani.. Alivyoniona akatulia kwanza, akanicheki huku akijiinua taratibu huku ulimi wake ukiwa unacheza cheza na domo lake leusi..
Aiseee, jasho lilitoka kama mvua, vinyoleo vyote vilisisimka nikaona mwisho wa maisha ndio leo..
Tukawa tunaangalia, sikupepesa hata jicho wala kusogeza kiungo chochote, nae akawa katulia tuu ananiangalia..
Nikaanza kusali sala ya Baba yetu moyoni na sala ya toba juu.. Tulikaa hivo kama dakika 5-10, nikaona huyo anaanza kujisogeza mdogo mdogo na kuingia machakani..
Nilitulia pale hadi akapotelea huko msituni, nikamwongezea dakika zingine ili afike mbali.. Nilichomoka hiyo spidi, breki ya kwanza kitandani na usingizi juu.. Haikuisha hata mwezi nikasikia kuna mtu tayari kashakobokolewa..