Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Duh poleni sana Wakwe na Shemeji zangu
 
Nasikia huyu ankali MAMBA ana kisasi sana anaweza akakaa chini yauvungu wa gari mpaka ahakikishe anaishi na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ni noma aisee, nilishaona clip mzungu ilikuwa amlenge akiwa anavuka barabara. Akasimama amngoje avuke. Kumbe jamaa hajavuka kapanda uvunguni kwenye engine kajisogeza hadi usawa wa mlango. Ile mzungu kaondoa gari tu kumbe kambeba. Jamaa anafika home tu na kupaki ndinga anafungua mlango ile anashusha mguu tu akapewa moja tu. Akajua kabisa ni yule black mamba waliomkwepa road kumbe alipanda gari akasepa nao.
 
Kwangu mi niliemuona Huyo kiumbe nahisi ndo shetani mwenyewe make si kwa akili na maarifa aliyonayo Koboko.
Hata mwili wa alieng’atwa na koboko ukiuparamia lile jasho likakugusa kufa hufi ila maluwe luwe au nyota utaziona tu
Nyoka wengi wana tabia ya kung’ata mara moja tu ila koboko sio mara 1 ana uwezo wa kung’ata mara nyingi ndani ya muda mchache tofauti na wengine!
Hauwi adui kwa ajili ya kitoweo/chakula la hasha huuwa kwa ajili ya kujimwambafai.
Mara nyingi huamua tu kukaa njiani makusudi, kwa wachungaji waweza swaga mifugo huku nyuma kumbe walio mbele washamuona wanagoma kwenda na koboko kitu hataki ni kero/ bugudha sasa kazi inabaki ni kugonga tu mifugo, hata gari analidindia kabisa.
Nyoka yo yote akimhisi binadam karibu na alipo hukimbia au kumkwepa kulingana na uadui Mungu aliouweka kati yetu na nyoka, cha ajabu koboko ye huo muda hana zaidi ya kuja ulipo.
Vile vile ana tabia ya kutokomea kichakani au kwenye nyasi ndefu then akawahi mbele kuhakiki au kujiridhisha kama huna nia mbaya yaani waweza kufikiri ulimuacha umbali wa 1km ghafla akakatiza kwa mbele yako.
Aweza vuka barabara na utaona kimkia kinapotea ghafla anainuka anatua katikati ya barabara, kwa ujumla ana mikongo mingi sana ambayo usipokuwa makini utaanzisha shari kitu akitacho.
Kutana na koboko katika harakati zake za kawaida, ila sio koboko aliekosa nafasi ya kumpanda koboko jike. (Koboko Mbabe ndo hupanda jike tu)
Lakini pia koboko ni mlaji mzuri wa mbegu za bangi (marijuan)
 
mmenikumbusha juzi hapa nipo home usiku unajua ss tunaokaa pembeni ya mji tunabahati ya kuonana na viumbe hivi kila mara..

sasa nimekaa zangu usiku mtoto atanikimbilia anasema nyoka mkubwa jikoni eeh nilipata ngazi, nikawah faster ile nachungulia hivi kitu cheusi kipo katikati ya jiko mara huyo kaingia kwenye matndoo usawa wa masinki nikasema hapa kazi ipo nyoka mkubwa urefu wa mkono ...

nikawaambia watoto wote watoke wakae mbali na wasipige kelele nikawa mlangoni natafakari cha kufanya nikasema hapa nisitumie marungu nitajiharaisha maisha hapo nilisha somaga mada kibao za manyoka hapa jf akilli yote naomba asiwe black mamba maana hadi wakati huo huyo nyoka hakumuona mtu kwa hiyo alikuwa hana wasiwasi ni kama alikuwa anafuata joto au aliona panya nadhani ..

haraka nikawaambia nileteeni mafuta ya taa yajae kwenye kopo la maji ya kunywa la nusu lita nikawa mlangoni namchora na kuakikisha na jua movements zake zote mule jikon nikatoboa kopo la mafuta kwa msumarijuu kwenye kizibo nikahakikisha mafuta yana presha kubwa ya km mita 6 au 7 mamb yte hayo nilifanya kwa spindi na kwa haraka bila yule nyoka kugundua km ameonekana

nyoka alijiroga akaingi chini ya sinki nakulikuwa na ndoo pale nikanyata hadi katikati ya jiko kwanza nikamwaga mafuta chini kwenye tailizi ya kutosha yakasambaa pote kazi ikabaki moja tu kumchokonyoa huko alipo ili atoke sasa balaa .. maana hujui atarukaje huko nilipuriza mafuta ya kutosha kwa spidi bila kuacha kule kwenye sinki km sekunde sita naona kitu hiki hapa nika sema nikilegea nitasababisha madhara kwa wengine ivyo nikakazadha kurusha mafuta akakurupuka huka ili atoke sasa weee... ile anatoka atambae akatambali mafuta akaona imeshakuwa soo akataka kunyanyuka kam atembee hewani sijui ndo haruke akashindwwa akajikuta katua tena kwenye mafuta nikamshindilia mengine juu ya mgongo alijibilingisha nikampa tena ya tumbooo nikaona taratibu anakuwa mpole anajikuja akasalimu amri kirahisi sana nikachukua ponti za nokauti bila kutumia nguvu mbwa wangu akaja kumalizia kazi iliyobakia..

ila swali nililobaki nalo yule nyoka aliweza kuingia mule ndani na wakati huohuo kuna tailizi yaani mwanzo nilipo muona alinifanya nishake kwanza thank kwa wadau humu kwa kutujulisha silaha za uhakika za kupambana na hawa viumbe mafuta ya nimeyakubali sana yani nilimmaliza kirahisi sana yule shwaine..
 
Ndo maaana kumbe. Akishakula mbegu za bangi anajiona yeye ndo simba,yeye ndo tembo,yeye ndo nyati.




 
Luna story Nilisikia kuwa paka nae ni mataalamu wa kuuwa nyoka ndan ya dk 0 jamaa alinambia ukimuona nyoka unamleta paka unamchonganisha au unampleka sehem ambayo nyoka yupo hats awe koboko hapa atasalimu amri maana paka anapenda sana zile staili za nyoka kuinua kichwa sijui kupanda juu no mda mfupi sana atawekwa chini ya ulinzi we utazika tu
 
Good presentation style..inavutia kusoma japo inatisha

Siyo Kila Kiuzwacho Sokoni Chafaa Kununuliwa
 
Una nyotaa ya nyokà.wewe.mpwaaa jipangee usijee uma.wanaoo
 
Nikiwa zangu same kijijini uko na mdogo angu nikiwa around 9years ..Mara paap panya kapita spidi..kushangaza anakuja mzee kasimamia mkia..Yuko spidi hatari..sekunde thelasini keshamkamata panya afu apo si tumekaa tunashangaa..akarudi tena kashika panya wake akasogea mita moja ad usawa wa mabega yangu uku mi namuangalia tu,,asee anatisha balaaa usoni..afu nayeye anatuangalia uku Sasa kasimamia nusu ya tumbo...alivoona hatuna madhara akateleza uyo mshenzi..Yani kwa jinsi alivomrefu na kasimamia tumbo.kwenye vichaka unamuona hata umbali wa mita 20...kubabake apo alivofka mbali ndo nikajitia van same kubeba mawe..wakati huo Yuko mbali na sikurusha ata jiwe...thanks GOD hatukuogopa alivopita kututisha maana sio kwa utashi wetu...
 

Ofcoz paka haogopi nyoka[emoji23][emoji23] nyoka akichubuliwa kdg tu hawez pona


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huwa natazama kipindi flan kinaitwa Snake in the city kule kwenye national geographic wild, kuna jamaa mmoja nadhani yuko South Africa anawakamata saaana hawaa, bilaa ubishi wowoteeee
Black Mamba ni nyoka mkorofi na anaengoza kwa sumu kali hapa Africa, ila story nyingi zinazomuelezea huyu mjomba zimejaa chumvi nyingi sana, yaani hata yeye mwenyewe angekua anajua kusoma makala zinazomzungumzia naamini angekufa kwa mshtuko wa moyo kwa kuona jinsi watu wanavyomsingizia.
 
Pamoja na nyoka huyu kuwa tishio Sana lakini kuna huyu mnyama hapa jamii ya panya anaitwa Mongoose, anakula black mamba..kama SOSEJI vile

Katika uumbaji hata kama mnyama ni mkali vipi lazima awe na mbabe wake humo humo porini


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…