Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Mambo ya Kutembea na Jungu achana na huo ujingaa mkuu... Vingine vyote point!!
 
Secretary bird kana miguu mirefu hivi yule ni kiboko ya nyoka.Watemi wengine wa nyoka ni honey badger na mangoose
mongoose anaweza akakimbia msosi akikutana na nyoka mbabe,ila huyo ndege ni balaa,ana miguu mirefu,anarusha mateke vibaya mno.
nyoka ndiyo msosi wake pendwa,siyo kama nyegere,anakula nyoka for fun tu.
 
Chungu cha moto kikikumwagikia?
Kofia ngumu je akikupapasa shingoni ushahisi kitakachokutokea mkuu?maana bora chungu akishuka akikigusa hata kwa bahati mbaya atakuta nacho ni cha moto atainuka juu hiyo kofia ngumu akiigusa si ndo atatelezea hapo shingoni.
 
mongoose anaweza akakimbia msosi akikutana na nyoka mbabe,ila huyo ndege ni balaa,ana miguu mirefu,anarusha mateke vibaya mno.
nyoka ndiyo msosi wake pendwa,siyo kama nyegere,anakula nyoka for fun tu.
Honey badger yeye akigongwa na nyoka anazimia baadae anananyanyuka
 
Tukiwa safarini kuelekea Karatu na Noah, kabla hatujafika mto wa Mbu. Mwanadada mweupe mmoja aliekaa mbele aliomba kushuka ili ajisadie. Akaenda kwenye vichaka karibu kwenye kichuguu cha mchwa. Hapo tuliona tamthilia ya aina yake.kwani mara tu tulisikia kelele na mwanadada yule alikuwa anarudi akikimbia huku chupi nusu mlingoti ikiwa inamkwaza na kumdondosha.Kinachomkimbiza ni nyoka wa kijivu mwenye hasira kali, cha kushangaza nyoka yule aliendelea kumng'ata yule Mwanadada zaidi ya mara moja. Gari nzima tulipaniki na hakuna alieshuka kumsaidia hadi tulipoona nyoka yule akiondoka huku kichwa kikiwa juu. Baada ya majibizano Kwa ushauri wa abiria mara afungwe sehemu alizong'atwa, mara mtu mmoja anyonye sumu, tutafute jiwe la nyoka n.k, vyote kumbe useless! Abiria walishuka na gari na mgonjwa wakarudi hadi Meserani snake park hapo kuna Ant-venom za nyoka aina mbalimbali. Hio ndio iliokoa maisha ya Abiria yule.
Angalizo
Usifunge sehemu kuzuia mzunguko wa damu juu ya jeraha au chini palipong'atwa na nyoka
Usinyonye sumu kwenye jeraha la nyoka. Unaweza kuwa na kidonda mdomoni usichokijua hapo madhara utayaona.
Jiwe la nyoka halisadii, wahi kwenye kituo cha tiba na ni vizuri ukawa na maelezo ya Jinsi nyoka alivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…