Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Huyu ni moja kati ya nyoka hatari zaidi duniani, pia ameusika kwenye vifo vingi vinavyohusishwa na nyoka. Kwa jina la kimombo ni "black mamba" sumu yake inashambulia mfumo wa Neva uchukuwa takribani dakika 10 kumuua binadamu. Huyu nyoka anaweza kufikia urefu wa mita 3 Yani futi 9 na inch 10. Ana uwezo wa kurudia kung'ata zaidi ya mara moja. Kwa hapa Tanzania wanapatikana sana mkoa wa Tabora na mikoa mengine yenye Hali ya joto joto. Anaweza kuwa na rangi ya brown na grey, jina la black mamba ni kutokana na ndani ya mdomo wake kuwa na rangi nyeusi. Hatari sana huyu nyoka ukimuona pita mbali sana usijaribu kupambana nae Wala usitumie fimbo kabisa..!!
 
Ndani ya mdomo wa Koboko aka blackmamba
Screenshot_20230128-204525_1.jpg
 
Mjue Nyoka Aina Ya Coboko*Au Black_Mamba
nyoka huyu ni miongoni mwa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani, ni nyoka anaependa sehemu tulivu isiyo na kelele, na ni mwepesi kubaini hatari yoyote pindi anapokuwa mawindoni na kuwa tayari kwa lolote, hata kama yuko mbali atajaribu kufika eneo analodhani ni hatari kwa uhai wake na kukabiliana nalo kikubwa ahakikishe yuko salama kwa asilimia mia moja, ana uwezo wa kuwagonga ng'ombe ishirini kwa dakika zisizo zidi tano, ni mwepesi wa kutoroka pindi anapoona kazidiwa na adui, na sehemu anayoishi haruhusu kiumbe chochote kuwa karibu, lakini pamoja na ubabe wake wote huo hana ujanja kwa ndege wanaoitwa bundi na mwewe weusi wakubwa huwa ni chakula pendwa kwa ndege hao, na ndiyo maana mawindo ya nyoka huyu huwa asubuhi kuanzia saa tatu mpaka saa tano na hurudi sehemu anayoiamini ni salama kwake ( kwenye pango au kwenye vichuguu) na mchana hutoka pindi jua limepoa na hufanya mawindo yake mpaka jua linapo anza kuzama tayari huwa katika sehemu salama, pia ni kiumbe asiyependa unyevu nyevu hivyo hulazimika kuhama pindi inapofika masika huhamia kwenye mapango ya miti na kiangazi hurudi kwenye vichuguu, kuna koboko wenye rangi tofauti tofauti lakini hawa wawili wa kijivu na rangi ya brown (kahawia) ni hatari sana.
Nb. Nyoka hawa huuma pindi utakavyo washtukiza ila kama watakuona umbali wa mita tano na hujamuona husimama urefu wa mita mbili na kukugonga kichwani, urefu wa hawa nyoka hufikia hadi futi kumi na mbili.View attachment 2498561
Thread gani hizi usiku huu na umeme hakuna
 
Kitu km hujui bora unyamaze..koboko alivyo na unavyomtaja ni tofauti kbs.rudi kasome articles zake then uje ku edit
 
Mjue Nyoka Aina Ya Coboko*Au Black_Mamba
nyoka huyu ni miongoni mwa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani, ni nyoka anaependa sehemu tulivu isiyo na kelele, na ni mwepesi kubaini hatari yoyote pindi anapokuwa mawindoni na kuwa tayari kwa lolote, hata kama yuko mbali atajaribu kufika eneo analodhani ni hatari kwa uhai wake na kukabiliana nalo kikubwa ahakikishe yuko salama kwa asilimia mia moja, ana uwezo wa kuwagonga ng'ombe ishirini kwa dakika zisizo zidi tano, ni mwepesi wa kutoroka pindi anapoona kazidiwa na adui, na sehemu anayoishi haruhusu kiumbe chochote kuwa karibu, lakini pamoja na ubabe wake wote huo hana ujanja kwa ndege wanaoitwa bundi na mwewe weusi wakubwa huwa ni chakula pendwa kwa ndege hao, na ndiyo maana mawindo ya nyoka huyu huwa asubuhi kuanzia saa tatu mpaka saa tano na hurudi sehemu anayoiamini ni salama kwake ( kwenye pango au kwenye vichuguu) na mchana hutoka pindi jua limepoa na hufanya mawindo yake mpaka jua linapo anza kuzama tayari huwa katika sehemu salama, pia ni kiumbe asiyependa unyevu nyevu hivyo hulazimika kuhama pindi inapofika masika huhamia kwenye mapango ya miti na kiangazi hurudi kwenye vichuguu, kuna koboko wenye rangi tofauti tofauti lakini hawa wawili wa kijivu na rangi ya brown (kahawia) ni hatari sana.
Nb. Nyoka hawa huuma pindi utakavyo washtukiza ila kama watakuona umbali wa mita tano na hujamuona husimama urefu wa mita mbili na kukugonga kichwani, urefu wa hawa nyoka hufikia hadi futi kumi na mbili.View attachment 2498561
Sema ni vile tu wanaadam mna nongwa sana. Mbonna msela yupo pisi sana. Kama hapo anajipungia zake upepo tu.
 
Back
Top Bottom