Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Mjue Nyoka Aina Ya Coboko*Au Black_Mamba
nyoka huyu ni miongoni mwa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani, ni nyoka anaependa sehemu tulivu isiyo na kelele, na ni mwepesi kubaini hatari yoyote pindi anapokuwa mawindoni na kuwa tayari kwa lolote, hata kama yuko mbali atajaribu kufika eneo analodhani ni hatari kwa uhai wake na kukabiliana nalo kikubwa ahakikishe yuko salama kwa asilimia mia moja, ana uwezo wa kuwagonga ng'ombe ishirini kwa dakika zisizo zidi tano, ni mwepesi wa kutoroka pindi anapoona kazidiwa na adui, na sehemu anayoishi haruhusu kiumbe chochote kuwa karibu, lakini pamoja na ubabe wake wote huo hana ujanja kwa ndege wanaoitwa bundi na mwewe weusi wakubwa huwa ni chakula pendwa kwa ndege hao, na ndiyo maana mawindo ya nyoka huyu huwa asubuhi kuanzia saa tatu mpaka saa tano na hurudi sehemu anayoiamini ni salama kwake ( kwenye pango au kwenye vichuguu) na mchana hutoka pindi jua limepoa na hufanya mawindo yake mpaka jua linapo anza kuzama tayari huwa katika sehemu salama, pia ni kiumbe asiyependa unyevu nyevu hivyo hulazimika kuhama pindi inapofika masika huhamia kwenye mapango ya miti na kiangazi hurudi kwenye vichuguu, kuna koboko wenye rangi tofauti tofauti lakini hawa wawili wa kijivu na rangi ya brown (kahawia) ni hatari sana.
Nb. Nyoka hawa huuma pindi utakavyo washtukiza ila kama watakuona umbali wa mita tano na hujamuona husimama urefu wa mita mbili na kukugonga kichwani, urefu wa hawa nyoka hufikia hadi futi kumi na mbili.View attachment 2498561
DAH koboko dude HATARI SANA kama CCM ya jiwe
 
Wewe huo muda wa kuzuga unatoka wapi wakat uho akili ishakutumuma kimbia haraka sana
Na unatakiwa ukimbie kwa adabu. Maana lilivyo na akili ya kiidikteta linaweza kudhani unakimbia kwenda kuchukua silaha... Basi linakufukuza kukushughulikoa

Kesho majirani wanakuwa wanafunga maturubai huku wengjne wakisema umeumaliza mwendo, vita umevishinda.... wengine wakisema Mungu amekupenda zaidi
 
Na unatakiwa ukimbie kwa adabu. Maana lilivyo na akili ya kiidikteta linaweza kudhani u akimbie kwenda kuchukua silaha... Basi linakufukuza kukushughulikoa

Kesho majirani wanakuwa wanafunga maturubai huku wengjne wakisema umeumaliza mwendo, vita umevishinda.... wengine wakisema Mungu amekupenda zaidi
Haoana mkuu mimi sioendi tembea porini wala sehemu nikihisi kuna nyoka umhuwa natembea kwa adabu sna
 
Chums kingine hiki hapa Kifutu aka Puff adder
Screenshot_20230128-210200.jpg
Screenshot_20230128-210124.jpg
 
Nilisikia habari zake nikamfuatilia kwenye documentaries... We ogopa kitu unakiangalia kwenye screen lakini unahisi kiko pembeni yako.

Senge lina kisirani na kisasi cha ajabu. Afu sumu yake linaweza kuua mtu hata 10 keimamae zake...
Hahahaa aisee
 
Very quick in reacting, quick in escaping and arrogant!

Linaonekana la kawaida lakini huwa halina muda wa kumheshimu mpinzani.
 
Back
Top Bottom