Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Nawapenda sana nyoka hata nikienda zoo lazima kwanza niulizie walipo

Ila huyo mwamba ni zaidi ya shetani yaani ana hasira za kipumbavu kama yule mwalimu mkuu

Natoka sehemu wanakozaliana sana huwa naomba nisije kukutana nae huyu kiumbe

Anaweza kuanza kukumbiza bila sababu, na ukiwa na Gari anasimama makusudi mbele, sasa jichanganye na wewe kama kawaida yetu kushangaa shangaa kwa kila kitu
Utamkuta chumbani kwako usiniulize kafikaje huko labda ulimpa lift

Maana anaona lazima una familia ndio maana anakufuata akawamalize wote
Hasidi mkubwa huyu
 
Huyu ni moja kati ya nyoka hatari zaidi duniani, pia ameusika kwenye vifo vingi vinavyohusishwa na nyoka. Kwa jina la kimombo ni "black mamba" sumu yake inashambulia mfumo wa Neva uchukuwa takribani dakika 10 kumuua binadamu. Huyu nyoka anaweza kufikia urefu wa mita 3 Yani futi 9 na inch 10. Ana uwezo wa kurudia kung'ata zaidi ya mara moja. Kwa hapa Tanzania wanapatikana sana mkoa wa Tabora na mikoa mengine yenye Hali ya joto joto. Anaweza kuwa na rangi ya brown na grey, jina la black mamba ni kutokana na ndani ya mdomo wake kuwa na rangi nyeusi. Hatari sana huyu nyoka ukimuona pita mbali sana usijaribu kupambana nae Wala usitumie fimbo kabisa..!!
Huwa mnatia chumvi sana!

Kuna yule jamaa kwenye kipindi cha snake in the city kwenye chanel ya wanyama huwa anawakamata kwa mkono tu

Ni kweli ni kiumbe hatari lkin yeye mwenyewe akikuona huwa anajificha ili kuokoa uhai wake
 
Yule jamaa ni mtaalam wa nyoka ndio kazi yake, kama unaona sio hatari jaribu wewe kumkamata. Najua Hiko kipindi kipo NatGeo Wild ni jamaa wa South Africa sikiliza maelezo yake vizuri kama yanatofautiana.
 
Umekurupuka sana, hamna koma wala nukta, pia nilitaraji kukutana na melezo mapya kumuhusu huyu kiumbe, ila ninayo yajua ni mengi kuliko niliyo yakuta humu
Sema yeye wakati anaandika, hakudhani kuwa wewe utasoma.
Ila siyo kila unachokijua sote tunakijua, hivyo acha waendelee kuandika tu, kwa faida ya wengine.
 
Huwa mnatia chumvi sana!

Kuna yule jamaa kwenye kipindi cha snake in the city kwenye chanel ya wanyama huwa anawakamata kwa mkono tu

Ni kweli ni kiumbe hatari lkin yeye mwenyewe akikuona huwa anajificha ili kuokoa uhai wake
Hadithiwa hivyo hivyo mkuu usiombe hata akutane na ndugu yako maana itakugharimu mazishi yake.

Yule jamaa mwenye ma-tattoo na wenzake wanakuwa vaccinated na snake venom japokuwa Black Mamba survived hupata utaahira wa maisha so huyo anayecheza nao kwanza analipwa mpunga mrefu pili ni mzoefu wa muda mrefu ikitokea akapata ajali atarudishwa shule kufundishwa ABCD maana sumu ya koboko huondoka na ufahamu wote.
 
Sema yeye wakati anaandika, hakudhani kuwa wewe utasoma.
Ila siyo kila unachokijua sote tunakijua, hivyo acha waendelee kuandika tu, kwa faida ya wengine.
Kuna nyuzi zaidi ya kumi humu ndani kuhusiana na hichi chuma, zina detail nyingi sana, hivyo kuona hii nikafikiri anaeza kua na kigeni, kumbe pumba tupu hata kupangilia story line hola, maandishi hola! Huyu kiumbe anaweza kua na maajabu mengi tusio fahamu hivyo unapokuja na uzi kama huu lazima tuvamie sasa unapo kuja kutulisha ma pushabu badala ya shada unakua hueleweki
 
Katika vitu huwa namuomba Mungu kila siku ni kutokukutana na hawa viumbe, awe na roho mbaya au peace, awe mtoto au mkubwa.
Hapa nimesoma mpaka nikijigusa naogopa. Watu wanasema hata kama unamchukia mtu kupitiliza usimuombee kukutana na koboko.
 
Kuna nyuzi zaidi ya kumi humu ndani kuhusiana na hichi chuma, zina detail nyingi sana, hivyo kuona hii nikafikiri anaeza kua na kigeni, kumbe pumba tupu hata kupangilia story line hola, maandishi hola! Huyu kiumbe anaweza kua na maajabu mengi tusio fahamu hivyo unapokuja na uzi kama huu lazima tuvamie sasa unapo kuja kutulisha ma pushabu badala ya shada unakua hueleweki
Ili kulinda umaana wako, uliposoma ukaona hana mpangilio wa uandishi, tena kaandika pumba.
Mbaya zaidi hizi pumba zimeandikwa zaidi ya mara kumi, Ungepita kimya tu.
Kama unadhani huyu nyoka, ana vitu zaidi ya haya yaayoandikwa, humu ni vizuri wewe ukayatafute utulee mkuu, sisi tutajifunza.
 
Uyo nyoka mbona ni wakawaida sana mara kibao uwa nakutananaye kwenye chocho lakini hakuna kitu ananifanya..ana tofauti na kinyonga😀😀😀
 
Nilikutana na nyoka mweusii anakatiz barabara nikarudi zangu huwa sitaki shari kabisa maana alipokuwa anaelekea palikuwa na ukuta
 
Ili kulinda umaana wako, uliposoma ukaona hana mpangilio wa uandishi, tena kaandika pumba.
Mbaya zaidi hizi pumba zimeandikwa zaidi ya mara kumi, Ungepita kimya tu.
Kama unadhani huyu nyoka, ana vitu zaidi ya haya yaayoandikwa, humu ni vizuri wewe ukayatafute utulee mkuu, sisi tutajifunza.
Meengi yamesha andikwa humu humu, fuatilia tu
 
Back
Top Bottom