Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko [emoji22][emoji22]
Huyu nyoka sitaki hata kumsikia!
Alimgonga jirani yetu akiwa shambani, yule mama alipatikana kesho yake akiwa tayari keshafariki na keshakakamaa, pale alipokuwa amelala yule marehem kulikuwa na mashimo kadhaa katika kupekua na kuchunguza ndan ya shimo mara aliyekuwa anachunguza ambaye n mme wa marehem naye akagongwa ndan ya dakika 15 naye akafariki! Ilibidi atafutwe mzee mmoja mwenye gobore then wakapakia goroli za pedals za baiskel kama mbdala wa risasi, yule koboko alikuwa amechachamaa vibaya, kichwa juu juu! Ilibidi auwawe kwa gobore ndipo miili ya marehem ilipochukuliwa!
Huku kigoma wapo sana hasa wilaya ya uvinza!

Msimu wa kumbikumbi usipende kusogelea kwa pupa kwenye vichuguu! Na pia kwenye mashamba ya bange ni hataree!
 
Ni heri iwe hadithi tu, achana kabisa na huyo nyoka.ni heri ukutane na simba dume aliyejishibia kuliko huyo mnyama
 
so sad jamani
 
Kutana na moja kati ya nyoka hatari sana duniani.

THE DEADLIEST SNAKE ON THE PLANET!
Anaitwa Mamba mweusi wa Africa
The African Black Mamba!
Anapatikana katika Bara la Africa tuu...
Ndie nyoka hatari kabisa! Anatoa sumu aina mbili na zote ni noooma! Anatoa sumu inayojulikana kama "Neurotoxin hii huathiri mfumo wa neva
Napia anatoa sumu nyingine aina ya Cardiotoxin hii hushambulia mfumo wa moyo.... Nyoka huyu akikuuma unaweza kufa ndani ya dakika 20!

Black Mamba ninyoka mkorofi katili anasumu kali, anasifa ya urefu kama uavyomuona anafika hadi miguu 14 kwa hesabu za kiswahili! Ye huwa hana mwili mkubwa kama kina Python(Chatu) Mungu ni fundi sana huwa hakosei! Huyu nyoka ana roho mbaya sana kwanza amejaaliwa mbio kuliko nyoka wote! Ukikutana nae kuna ishara kuu mbili atakuonyesha kuwa Mimi African Black Mamba... Nyoka niliye jaaliwa sumu kuliko nyoka wote! Ulaya hayupo huyu lkn Wazungu wanamtambua vema wakotaka kuja Afrika kuna viumbe kwanza wanaambiwa mkifika huko mnapaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu na viumbe hivi hatari.. Ktk list huyu nae yumo! So ukipata bahati yakukutana nae kwanza atakutisha! Ata achama kinywa ama mdomo wake wenye rangi nyeusi kwa ndani! Kinywa chake ni cheusi kwa ndani na ndio kimefanya aitwe Black Mamba! Pili utamskia anatoa sauiti kama msela anaita demu! Au kama tairi linalotoa upepo...Tatu utamuona anatanua shingo yake japo c kama ya Cobra!!! Hapo ujue uko mbele ya nyoka hatari kabisa! Uzidishe maombi! Vitu viwili usijethubutu kuvifanya! Moja... Uskimbie.. Maana huyu nyoka anambio zaidi ya Husein Bolt! Mamba anakimbia Maili 12 kwa saa... Na akikumbiza hakubali hadi akugonge sehemu ya mwili wako.. Ye ardhini huwa anateleza! Na ukimkimbia ni lazima tuu atakuunganishia! Na hatakukosa! Pili kuna wale watu akiona tu nyoka ye anakimbilia fimbo au jiwe... Siku ukutana na nyoka huyu jua umekwisha! Wataalam wanakwambia nyoka huyu hapigwi! Kwani hata hilo jiwe huenda usiwahi kulirusha au mfe wote! Kwani Black Mamba anasifika kwa Show za kikatili anashambulia vibaya sana! Ndio maana nilisema Mungu nifundi! Pamoja na kumuumba nyoka huyu na Sumu kali mbio nyingi, hasira na urefu lkn hapo hapo nyoka huyu amejaaliwa huruma ndani yake ukikutana nae akianza kukuonyesha sarakasi zake kuwa mimi ndie nyoka hatari nawe Binaadam ukijishusha uskimbie wala ustupe jiwe ubaki unamuangalia tuu macho kwa macho! Unaambiwa atatuliza mzuka! Na wala hatakugusa ataingia zake mitini! Unaona Muumba alivyo wa ajabu!! Mamba anataga mayai kama kuku tuu kiota chake huwa ardhini...Jike anataga mayai 10-25 akishataga mayai yake huwa yanajiengua yenyewe tuu baada ya miezi mitatu....Joto ni muhimu kwaajili ya lncubation...na vitoto vyake vikisha jitotoa unaambiwa vinaanza mishe saa hiyohiyo hujitegemea kwa kilakitu! Na vinakuwa na sumu kali kama Mama yao tuu yaani haina kuremba!!! Nyoka huyu anaishi hadi miaka 11 porini... Akiwa anafugwa anaeza ishi hadi miaka 12...... Mi nilishawahi muona huyu nyoka michezo alituonyesha imenifanya nisitamani kukutanae tena japo nawapenda wanyama na wadudu!!.

Picha na stori toka kwa Faru Wa Kikwete
 
Black mamba=Mamba mweusi
Hivi kuna mamba mweupe,kijani au rangi nyingine tofauti na nyeusi?
 
Mbn haujaweka picha sasa hata tumfahamu kwa picha tu
 


NIMEGUNDUA YAFUATAYO

Jina [HASHTAG]#blackmamba[/HASHTAG] limetokana na ulimi wake kuwa mweusi sana. Pia anaitwa koboko #2 blackmamba hurusha mate na kulenga hadi umbali wa mita 5, #3 sumu yake humuua binadamu ndani ya dakika 20, #4 blackmamba ana uwezo wa kuwagonga hadi watu 100 mfululizo bila kuchoka #5 blackmamba hukimbia hadi kilometa 27 kwa saa.

#6 blackmamba akitaga mayai kamwe harudi kuangalia maendeleo yake, huyaacha mpaka yanajitotoa yenyewe. #7 kinda la blackmamba linapototolewa tayari huwa lina sumu ya kumuua mtu mmoja. #8 blackmamba akipandwa na hasira hutoa sauti kama ya tairi inapotoa upepo!! Huko @Australia kuna blackmamba wa kupaa! #9 koboko akipambana na nyegere na mbweha hupata shida. [HASHTAG]#Nyegere[/HASHTAG] akiingiwa na sumu ya blackmamba hufa na baada ya dakika 30 huzinduka na kurejea hali ya kawaida na kuanza mapambano upya. [HASHTAG]#Watu[/HASHTAG] waliowahi kung'atwa na blackmamba baada ya miaka 30 huja kuwa vichaa! [HASHTAG]#blackmamba[/HASHTAG] kama hajakuona wewe usikurupuke kukimbia, tembea taratibu uende zako!
 
Nyoka huyu ujulikana kama KOBOKO au Black Mamba.
hupatikana katika sehemu za Mashariki na Kusini mwa Afrika huishi katika Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu.
Nyoka huyu akitaka kufanya shambulio hutanua kinywa chake na shingo yake na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa linatoa upepo.
Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa (Neuro) hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni (Cardio-toxin) hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza kuua binadamu chini ya dakika 20.
Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake yanaweza kuua lakini mbali na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, Koboko hana ujanja mbele ya Nguchiro,Mbweha, na Nyegere.
 
so mzee wa magogoni anataka tuwe na kasi kama uyo nyoka heeeeh

iyo inaitwa speed ya light
 
Koboko siyo yule mwenye mapembe adder? Nilidhani huyu ni Swila au enchwela kwa lugha zetu. Adder yule anakufukuza hata akichukia. Sijui kuweka picha ningemuweka ila huwa mkia wake untoa sauti. Nikosoe lakini maana lugha gongana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…