Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Yuko na mwanasayansi mmoja mmarekani mwenye asili ya ujerumani alikuwa anamchezea Boomslang mdogo akang'atwa alipoulizwa kama asaidiwe matibabu akasema nyoka huyo ni mdogo kwa hiyo hana madhara...alikufa usiku wake.
Boomslang kwa kiswahili ni?
 
Huyo black mamba ndio koboko ni lugha tu hiyo
Huwa nasikia kuwa anagonga kichwa na hicho chungu
Kwa technology ya sasa itabidi tuweke camera
Haitashindikana najua wataalamu wamo humu
 
NIKIKUTANA NAYE BARABARANI NIFANYEJE JAMENI????? MAANA NINA TABIA YA KUFUKUZA NYOKA KWA MAWE AU GONGO.🙁
Kitu nilichojifunza kuhusu koboko ukikutana nae polini okota tofali au jiwe lolote kisha liweke kichwani haraka haraka hivyo akija kugonga kichwani atagonga jiwe au tofali .

Kama hakuna tofali okota mti au tumia gongo uanze kupambana nae ukiona amekurukia kichwani au anakuja mpige na gongo kumzuia asigonge utasoni na wakati unapambana nae usiwe muoga yaani wee hakikisha unalinda kichwa chako tuu na katika mapambano yako hakikisha unamtaja mungu wako akusaidiee koboko akuone huruma akusamehee maana yule mdudu huwa hawezi kusalender katika mapambano
 
Koboko anagonga popote pale hili la kusema anatafuta kichwa tu sio kweli labda akiwa kwenye mti na wewe unapita

Na mda wote hayupo mtini
 
Kweli Mwenyez Mungu kila upande kaweka maaajabu yake, tembo wanaomboleza km binadamu, tembo analia kwa uchungu
 
Huko South afrika wakati wa utawala wa makaburu walikua wanachukua mayai yake yakishatotolewa wanawafuga kidogo halafu usiku wanaenda kuwaachia kwenye maeneo ya weusi cha ajabu wale koboko walikuwa ni wapole mpaka leo koboko ni wengi kwenye miji yao.
Hahhhahahha, we jamaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…