We!
Tembo kwa visasi usimtanie kabisa.
Kuna Daktari Mzungu wa wanyama pori alkuepo pale mikumi,
naskia aliwahi kuuawa na Tembo kikatili sana.
Jamaa naskia alikuta kitoto cha Tembo kiko hoi bin taabani peke yake pirini kimepona pona kuuwawa na Simba.
Basi jamaa akaita gari kikapakiwa na kupelekwa camp kwa matibabu.
Kilipopata nafuu,
Na kuweza kusimama na kutembea.
Majamaa wakaona ni vema kikarudishwa tu porini kiendelee na maisha yake.
Basi wakakipakia Tena kukirudisha porini.
Wakashauriana na wenzie kua NI vema kikapelekwa walipo jirani na Tembo wenzie kwa ajili ya Usalama wake zaidi.
Basi,
kikafikishwa na kuwekwa kama mita 500 kutoka walipo Tembo wenzie.
Basi wakaona kimesimama tuli na wenzie wanaanza kukifata
Wenzie wakawa kama wanakifariji na kama wanacheza hivi
Mda so mrefu wakaona kimelala chini, jamaa wakahisi labda ndo michezo yenyewe.
Baada ya hapo,
Tembo wenzie wakaanza kutoa sauti kubwa sana.
Yule dokta akawaambia wenzie kua,
Inawezekana hali ya kile kitoto ni mbaya zaidi.
Huo ni mlio wa huzuni kwa tembo kulia vile.
Ni vema wakasogea na kuangalia zaidi,
Jamaa wakasogeza gari karibu mpk kufkua km mita 200 hv.
Ghafla Jamaa wakawaona tembo wakichimba shimo pana.
Yule Dokta akawadokeza wenzie kua,
"Bila shaka kile kitoto cha tembo kitakua kimefariki, hayo yatakua ni maadalizi ya mazishi"
Basi dokta akawasihi,
"Ni vema tutoke hapa HARAKA sana, tembo huwa hawataki kabisa bugudha wakati wa mazishi"
Wale jamaa wakang'ang'ania eti wanataka waendelee kuona mpaka mwisho jinsi Tembo wanavyofanya mazishi.
Basi jamaa wakanogewa kuendelea kuangalia lile tukio.
Basi mwenzao mmoja, akachomoa kamera ili kupiga picha.
Aisee;
Ile jamaa alipopiga picha moja tu, ule mwanga wa flash ukawapiga wale tembo.
Ghafla waliona tembo wawili WAKUBWA wakiwageukiwa na kuja kwa kasi ya ajabu.
Yaan ile hata gari kubwa waliokua nayo (mitsubishi fuso) haijawaka, wale tembo waliipiga kwa nguvu ikayumba.
Wakaipiga Tena, ikapinduka.
Ghafla wakaona washafika tembo kama 5 hivi.
Wakaendelea kuipiga, gari ikaanza ku-roll mpaka kwenye kwenye mfereji wa maji.
Basi ilkua kila aliepata upenyo, ni kukimbia tu. Mpaka silaha zao walisahau kwny gari lile.
Jamaa wenzie walioweza kutoroka, kwa mbali walimuona aliebaki pale ni dokta.
Na keshatolewa nje ya gari anakimbizwa na Tembo wawili
Na kwa sababu, eneo LA camp halikua mbali, jamaa wakakimbilia camp kuchukua silaha kumsaidia dokta.
Wanarudi tu,
Wakakuta tembo washaondoka na dokta ndo keshauwawa tayar na kazikwa kwnye shimo fupi Jirani na kile kitoto cha tembo na kufukiwa kwa majani&matawi ya miti.
Waliitoa maiti ya dokta kwenye shimo ikiwa imevunjwa vunjwa viungo vyote.
Na ikiwa haina mkono mmoja.
DAH; JAMAA WALIUMIA SANA.
WAKAJILAUMU SANA KWANINI HAWAKUFATA USHAURI WA DOKTA KUA WAONDOKE ENEO LILE HARAKA SANA.
WAKAMLAUMU SANA MWENZAO ALOPIGAILE PICHA YENYE FLASHI NA KUWAAMSHA GHADHABU TEMBO.
WAKAWAZA KUA ,
HUENDA TEMBO WALIFANYA KISASI WAKIHISI YULE DOKTA NDO KASABABISHA KIFO CHA MWENZAO.
INAWEZEKANA NDO MAANA WALIPOMUUA WALIENDA KUMZIKA JIRANI NA KITOTO CHAO
Dah, Jamaa wote waliumia sana.
( Hii stori nlisimuliwa na Mzee Mose, alkuaga askali wanyama pori pale Mikumi. Kwa sasa amestaafu)