Black Mamba haina maana ni mweusi wapo wa kijani na rangi zinazoshabihiana na mazingira na bado ni black Mamba.
Kuna aina anuai za sumu za nyoka
1. 'Neurotoxin'
Hii ni sumu inayoathiri mfumo wa fahamu kwa maana ku paralyse mfumo mzima
Kwa lugha rahisi inakata mawasiliano ya mfumo mzima wa fahamu
Athari zake ni kauthiri mfumohewa na maeneo yanayotegemea mfumo wa fahamu kama moyo
Sidhani kama ni sahihi kusema kuna cardio-toxin, bali kuna sumu (venom) ambazo ni toxic kwa heart kwasababu ya kuingilia mfumo wa fahamu
2. Kuna 'Hemotoxin'
Sumu ya nyoka wa aina hii huathiri mfumo wa damu kwa kuingilia uwezo wa viwambo(membrane) kuzuia uvujaji wa damu maeneo ya mwili. Mwathirika huvuja damu
3. Cytotoxin
Hawa wanaathiri cells za mwili. Athari zake zipo eneo aliloumwa mwathirika.
Kama ni mkono haichukui muda utaona una malenge lenge, unaanza kuoza na kuathiri mwili kutokana na kidonda. Nyoka maarufu katika kundi hili ni kifutu
Ingawa kuumwa ni ajali na hakuna ajali nzuri, hata hivyo uwezekano wa mtu kupona unaanza na kundi la 3.
Ikitokea kuna ucheleweshaji wa mgonjwa, huenda akapoteza kiungo
Halafu ni 'hemotoxin' ambao wanatoa lau muda wa kutafuta mbadala kabla ya tamati
Kundi la kwanza ni baya sana 'linakata umeme' wa mwili. Nusu saa huwa muda mrefu
Katika haya ya nyoka yapo mengi sana ya kuelezwa
Swali tusilojiuliza ni 'je hospitali zetu zina anti-venom' ikitokea tatizo tatizo?