Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Nimesoma tokea mwanzo wengi mmetoa ushuhuda wa black mamba bite ila hakuna hata mmoja aliye toa somo la endapo uking'atwa first unatakiwa ufanye nini ili poison isiendelee kusambaa mwilini shame on you wakuu
Kunywa mkojo wanavyosemaga wazee wa ujiji Kigoma hapa..
 
Nimesoma tokea mwanzo wengi mmetoa ushuhuda wa black mamba bite ila hakuna hata mmoja aliye toa somo la endapo uking'atwa first unatakiwa ufanye nini ili poison isiendelee kusambaa mwilini shame on you wakuu
MIMI NINAVYOONA KAMA TUNAVYOVAA KONDOM KUJIKINGA DHIDI YA UKIMWI BASI ELEMENT KICHWANI YA PIKIPIKI KUJIKINGA NA KICHWANI NA KOBOKO
 
Wanachomaanisha wasemaji kama nimewaelewa Simba na Chui unaweza kukutana naye kama hana njaa au stress akakukaushia. Ila huyu mdudu ni kama asidi hana sababu. ukikutana naye piga sara ya mwisho haijalishi umemchokoza ana njaa hana njaa yeye anatamani awe pekeake pasiwe na kiumbe mwingine karibu yake. Ndio maana ya uhatari wake kuliko simba maana simba wengi hawawezi kupanda miti wala kuogelea ndani ya maji but huyu mdudu ni all weather panda mti ingia kwenye maji kimbia atakukamata tu. kama nimekosea mnirekebishe maana simfahamu wala sijawahi kumuona na Mungu aniepushe naye.

Huu uzi kwa sisi waoga wa nyoka ni full kuogopeshana tuu.
 
Hii Mada ina mchanganyiko sana wa aina za nyoka, black mamba ni nyoka Mwenye aibu "mstaarabu", hukimbia watu, na asilimia kubwa ya nyoka waliopo Tanzania has a maeneo ya joto ni hawa, ila akidhani amezingirwa hushambulia kwa kujihami, ana sumu mbaya sana, lakini huyu sio koboko, cobra wala kifutu, Mara nyingi ana rangi ya kijivu, asubuhi unaweza za kumuona anaota jua njiani akikuona anajifungua taratibu na kuondoka.

Hawa wanaosema wanakimbizwa na nyoka huyo ni cobra, cobra hata kama ametotolewa Leo atazuia njia usipite, yuko tayari kufa kuliko kukimbia, akiwa Mkubwa anaweza kukimbiza kundi la watu.

Sasa watu wamechanganya koboko na black mamba ambaye ni nyoka anayepatikata kila mahali
Aisee..
 
images-9.jpg

Mkao wa kujihami.
 
Huko nyumbani kuna kijiji kinaitwa Koboko kutokana na huyo nyoka.. Kila mara lazima usikie mazishi, chanzo ni koboko.. Nilikuaga nasikia stori zake tuu, ila sikumtilia maanani..

Siku hiyo natoka sehemu fulani nikakatiza kwenye hicho kijiji ili nitokee kijiji chetu, kuna kanjia kanakatiza msituni na mto.. Sina hili wala lile, narusha mikono huku na kule natembea kwa raha zangu..

Hamadi!! Mita kama 4-5 toka nilipokuwepo nikamuona koboko rangi ya kijivu na weusi katanda njiani.. Alivyoniona akatulia kwanza, akanicheki huku akijiinua taratibu huku ulimi wake ukiwa unacheza cheza na domo lake leusi..

Aiseee, jasho lilitoka kama mvua, vinyoleo vyote vilisisimka nikaona mwisho wa maisha ndio leo..
Tukawa tunaangalia, sikupepesa hata jicho wala kusogeza kiungo chochote, nae akawa katulia tuu ananiangalia..

Nikaanza kusali sala ya Baba yetu moyoni na sala ya toba juu.. Tulikaa hivo kama dakika 5-10, nikaona huyo anaanza kujisogeza mdogo mdogo na kuingia machakani..

Nilitulia pale hadi akapotelea huko msituni, nikamwongezea dakika zingine ili afike mbali.. Nilichomoka hiyo spidi, breki ya kwanza kitandani na usingizi juu.. Haikuisha hata mwezi nikasikia kuna mtu tayari kashakobokolewa..
 
Natamani uendelee..

Alikuwa mkubwaa?
 
Hujasema ulipokutana nae ulifanyaje, mana umeishia kuita fimbo
Nilipoagiza fimbo na kuona inachelewa nikaanza kurusha mawe, akaondoka zake

Pia Bi Mkubwa alishawahi kutana nae alipomuona tu nyoka nae akasimama sasa Bi mkubwa kwa taharuki akataka kukimbia ila bahati akajikwaa na kupoteza fahamu hivyo yule Nyoka hakumng'ata, alisaidiwa na wasamalia wema alirudishwa mpaka Nyumbani huku akiwa amevunjika mkono wa kulia,

Ila ukweli hawa Nyoka ni hatari sana na ni Wakorofi yaani ukikutana nae njiani inabidi ujihami kumuua ukisema ukimbie anakuua,
Maana hawajui kuogopa Binadamu na mara nyingi wanapenda kukuvaa uso kwa uso,

Mfano upo kwenye safari zako ghafla unakutana nae akivuka njia kutoka upande mmoja kwenda mwingine, akikuona usitarajie kwamba ataendelea na safari yake lazima atasimama msalimiane kisha ndo aende zake,

Kwa sisi tulioishi kijijini tunajua tu namna ya kuwatimua kama yupo ndani ya nyumba yako
 
Huyu nyoka namtunuku medali ya dhahabu ya Olimpiki. Pumbavu sana huyu mdudu...
Natamani Wizara ya Maliasili imfanyie promo nyoka huyu awe ni miongoni mwa vivutio vya utalii maana ni nyoka mwenye hadithi nyingi na hupatikana sehemu chache tu duniani ikiwepo Tanzania. Kinyume chake hua wanuwawa sana na muda si mrefu ujao wanaweza kutoweka kabisa
 
Nimesoma tokea mwanzo wengi mmetoa ushuhuda wa black mamba bite ila hakuna hata mmoja aliye toa somo la endapo uking'atwa first unatakiwa ufanye nini ili poison isiendelee kusambaa mwilini shame on you wakuu

Hawaamini kuna kupona uking'atwa!
 
Koboko ni kiboko sawa, ila kuna "chumvi" nyingi. Nimekutana nae aliyekomaa mara 2 porini. Mara moja nilitimua na hakunifukuza!
 
usiku huyo anawika kama jogo ni nyoka hatari sana usiombe ukutane nae akikuona hakimbii yeye anakufuata ulipo tofauti na nyoka wengine wanaogonga kwa bahati mbaya
 
Natamani Wizara ya Maliasili imfanyie promo nyoka huyu awe ni miongoni mwa vivutio vya utalii maana ni nyoka mwenye hadithi nyingi na hupatikana sehemu chache tu duniani ikiwepo Tanzania. Kinyume chake hua wanuwawa sana na muda si mrefu ujao wanaweza kutoweka kabisa
Hapana... acha tukose watalii... Huyu nyoka ni wa kuangamiza.

Shenzy kabisa huyu mdudu...
 
anatoka nduki balaa..................

nahisi hata mfupa wake ukukanyaga au magamba yanaweza kukudhuru
Nasikia wanapatikana sana Tabora, mi kwenda Tabora labda nibebwe na greda la Manispaa...

Acha niendelee kuitwa mwanaume wa Dar...

Potelea mbali!
 
uyo mzee alikuwa anapoteza muda....huko kijiji cha Mswaa korogwe izo shughuli zinafanywa na watoto wa shule ya msingi wanacheza nae mpaka wanamkamata na kumuua.
Unamzungumzia koboko aliekomaa au kifutu! acha kupotosha koboko hajawai kua fala kiivyo
 
Back
Top Bottom