Kocha Amunike atangaza majina ya Wachezaji watakaoenda kupambana na Uganda, Septemba 8

Kocha Amunike atangaza majina ya Wachezaji watakaoenda kupambana na Uganda, Septemba 8

Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko .

Taarifa za vyombo vya habari zinaeleza kwamba Kocha mpya wa Taifa Stars ameteua wachezaji watakaovaana na Uganda Cranes kwa michuano ya AFCON , sasa mimi ninataka kujua kama kweli aliyeteua kikosi hiki ni Amunike amewajuaje wachezaji wazuri bila hata kuwaona uwanjani ? nauliza hili ili matokeo mabaya yakitokea tujue wa kumpa lawama.

Msimchagulie timu halafu mkasema kachagua yeye , mwisho wa siku akatwishwa lawama kwa mtindo wa kuangushiwa jumba bovu , maana hata kwa akili ya vikatuni si rahisi kwa muda mfupi namna hii Amunike aweze kuwajua wachezaji , vinginevyo tutajieni mtu halisi aliyeteua timu hii .
Sina shaka kabisa kwamba wewe ni miongoni mwa wanataaluma wenye ueledi sana wa mambo ya habari na mchango wako ni mkubwa sana humu JF. Naomba unieleze kama taifa stars imevunjwa lini? Maana naamini Amunike kuna timu kaikuta sasa itabidi aifanyie kazi na maboresho, just like what happened to Spain after hierro took over
 
Basi labda wabadili lugha , badala ya kuteua wachezaji waseme Amunike aanza kazi Stars , maana si timu aliikuta tu ? Kuhusu Spain kilichotokea ni kwamba Hierro alichukua nafasi ya kocha aliyetimuliwa timu ikiwa tayari kwenye michuano .
 
Kocha mpya kwa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha Wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON dhidi ya Uganda

Majina ya Wachezaji hao yaliyotangazwa leo Agosti 21 ni Aishi Manula, Mohammed Abdilrahman, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Hassan Kessy na Gadiel Michael

Aidha, wengine ni Abdi Banda, Kelvin Yondani, Aggrey Moris, Andrew Vicent, Himid Mao, Mudathir Yahya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Saimon Msuva na Shiza Kichuya

Wachezaji wanaokamilisha orodha hiyo ni Rashid Mandawa, Farid Mussa, Hassan Dilunga, Feisal Salum, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu, John Bocco, Shabani Chilunda na Yahya Zaydi

Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Uganda mnamo Septemba 8, 2018
Wakapambane tu.
 
Sina shaka kabisa kwamba wewe ni miongoni mwa wanataaluma wenye ueledi sana wa mambo ya habari na mchango wako ni mkubwa sana humu JF. Naomba unieleze kama taifa stars imevunjwa lini? Maana naamini Amunike kuna timu kaikuta sasa itabidi aifanyie kazi na maboresho, just like what happened to Spain after hierro took over
Mkuu ww mpira hujui... timu ya taifa huwa sio permanent... eti walioitwa game iliyopita ndio wale wale.. hiyo hutokea katika mashindano tu.. mfano WORLD CUP YENYEWE AU AFCON YENYEWE SIO KUWANIA KUFUZU.. HIVYO WACHEZAJI HUBADILIKA KULINGANA NA MECHI NA MAONO YA KOCHA.. KUVUNJWA KWA TIMU YA TAIFA NDIO NN HAPO SASA..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ulitaka kutoa ushauri gani. Hebu saidia ungekuwa wewe ungefanyaje?

Hao wachezaji kawajuaje uwezo wao??? 🤔 🤔 🤔 Hakuna timu hapo na kila siku tutaendelea kubeba watu walewale walioshindwa kupanda mlima siku zote.
 
Back
Top Bottom