Kocha avua nguo uwanjani

Kocha avua nguo uwanjani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
SHIRIKISHO la Mpira wa miguu Zanzibar (ZFF) limemfungia miezi sita na kumpiga faini ya Sh 500000 kocha wa timu ya Miembeni Suleiman Mohamed kwa kitendo cha utovu wa nidhamu.

Juzi wakati timu yake ikicheza na timu ya Taifa Jang’ombe katika Uwanja wa Amaan, mchezo wa ligi daraja la kwanza kanda ya Unguja baada ya timu yake kushinda bao 1-0, kocha huyo alishangilia na kushusha suruali chini na kubaki na nguo ya ndani mbele ya mashabiki.

Kwa mujibu wa barua ya adhabu hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Kamati ya Mashindano ya ZFF Hussein Ahmada, wametoa adhabu hiyo kwa mujibu kifungu namba 31 cha kanuni ya kuendesha mashindano hayo.

Hussein alisema kocha huyo atatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya kipindi anachotumikia adhabu hiyo na akishindwa kulipa faini adhabu itaendelea mara mbili.

“Tumesikia kabla ya mchezo huo kocha huyo aligombana na mashabiki lakini sisi adhabu tuliyoitoa ni kufanya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu ambacho kimezagaa katika mitandao ya kijamii”, alisema Ahmada

. Pia Shirikisho hilo limeipiga faini ya Sh 100,000 timu ya Miembeni kwa kushindwa kumdhibiti kocha wao wakati akifanya vitendo hivyo na kusema vitendo vilivyofanywa na kocha huyo havikubaliki katika soka na hata mila na tamaduni za Kizanzibar.

Aidha ZFF imewataka viongozi wa timu hususani benchi la ufundi na mashabiki kuacha tabia ya utovu wa nidhamu pale timu zao zinaposhinda au kufungwa badala yake wazingatie kanuni za mashindano.

Chanzo: HabariLeo
 
😆😆😆😆 ilikuwa sio fair kabisa walichomfanyia lakini mtu kapandwa na midadi (mizuka) kwann asifanye yale wakati huo mtu yupo kwenye emotional nyingine kabisa.
 
Mi sijaelewa adhabu iliyopewa timu? Yaani walitakiwa wamshikilie asivue hiyo suruali au?
 
Back
Top Bottom