Kocha Banyai hatakiwi kukanyaga ardhi ya mji wa Njombe

Kocha Banyai hatakiwi kukanyaga ardhi ya mji wa Njombe

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Mashabiki wa soka wana mambo yao,baada ya Kocha wa timu ya Njombe Mji Banyai kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wowote ule wa ligi kuu mashabiki wa Njombe mji wameibuka na kumpa kocha lawama na kumwambia hatakiwi kukanyaga ardhi ya Njombe kama anajipenda.

Pamoja na yote hayo kocha Banyai ameonekana hana utani na maisha yake baada ya kujiuzulu kufundisha timu hiyo inayotumia uwanja wa Sabasaba uliopo Njombe Mjini akitoa taarifa kupitia kipindi cha Mshikemshike kinachorushwa na Azam Tv Kocha Banyai ameutupia lawama uongozi mzima wa timu ya Njombe mji na kusema wameshindwa kutekeleza mapendekezo yake ikiwa na pamoja na Kambi,usajili na pia Usafiri.

Kwa sasa Timu ipo mikononi mwa kocha Mlange kabange,Njombe mji wameweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufukuza kocha wake je Mlange Kabange ataweza kukidhi haja ya Wakazi wa Njombe? Time will tell.
 
Bado sana mambo ya zaidi ya kale hao
Mpira ni fair play wawe wavumilivu tu.
 
Hao nao ni waajabu kweli! Mechi 3 tu unafukuza mwalimu? Tena timu yenyewe hata usajili ulikuwa wa kuungaunga! Wasipojiangalia watarudi walikotoka, walidhani kucheza ligi kuu ni jambo dogo?
 
Hao nao ni waajabu kweli! Mechi 3 tu unafukuza mwalimu? Tena timu yenyewe hata usajili ulikuwa wa kuungaunga! Wasipojiangalia watarudi walikotoka, walidhani kucheza ligi kuu ni jambo dogo?
Wamecopy na kupaste kutoka Matopeni SC
 
Wamecopy na kupaste kutoka Matopeni SC

wamekopi vipi kwa unaowaita wa matopeni wekeni rekodi makocha wangapi walikimbizwa Yanga kwa kufungwa na Simba? nakumbuka wanne: Micho, Chamangwana, kuna mzungu mmoja alitokea Rwanda, Marcio Maximo huyo alikuwa Yanga tangu akiwa timu ya taifa, yaani nia yao ilikuwa unifying Young Africans and the National Team? Tanzania Bwana!
 
Back
Top Bottom