Kocha Julen Lopetegui aliyefukuzwa Uhispania na Real Madrid ateuliwa kuinoa Sevilla

Kocha Julen Lopetegui aliyefukuzwa Uhispania na Real Madrid ateuliwa kuinoa Sevilla

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Julen Lopetegui(52) amepewa kandarasi ya miaka mitatu kuinoa Klabu ya Sevilla ya Uhispania inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo

Alifukuzwa kuinoa timu ya Taifa ya Uhispania siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kuanza baada ya kuteuliwa kuwa Kocha wa Real Madrid

Mwezi Oktoba mwaka jana ikiwa ni miezi minne na nusu tangu ateuliwe kuinoa Real Madrid alitupiwa virango na Klabu hiyo kufuatia kipigo cha goli 5-1 kutoka kwa Barcelona

Sevilla iliyomaliza ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ilimfukuza aliyekuwa kocha wake, Pablo Machin mwezi Machi mwaka huu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Europa na kumteua Joaquin Caparros hadi mwisho wa msimu
IMG_20190604_134039.jpeg
 
Wameanza kuweweseka baada ya kufungana magoli mengi Na Simba Sport Club
 
Julen Lopetegui(52) amepewa kandarasi ya miaka mitatu kuinoa Klabu ya Sevilla ya Uhispania inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo

Alifukuzwa kuinoa timu ya Taifa ya Uhispania siku mbili kabla ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kuanza baada ya kuteuliwa kuwa Kocha wa Real Madrid

Mwezi Oktoba mwaka jana ikiwa ni miezi minne na nusu tangu ateuliwe kuinoa Real Madrid alitupiwa virango na Klabu hiyo kufuatia kipigo cha goli 5-1 kutoka kwa Barcelona

Sevilla iliyomaliza ya 6 katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ilimfukuza aliyekuwa kocha wake, Pablo Machin mwezi Machi mwaka huu baada ya kutolewa kwenye michuano ya Europa na kumteua Joaquin Caparros hadi mwisho wa msimuView attachment 1117347
Laana ya usaliti inamuandama..... Alikiwa na tamaa ya kutaka vyote Spain na Madrid kwa wakati mmoja.... Kilichotokea amekosa vyote. Hili liwe fundisho kwa makocha na wachezaji wengine wenye tamaa za mafanikio ya haraka badala yake wanatumbukia kwenye aibu kubwa.

Pole yake, hope amejirudi na kuwa committed kwa timu moja
 
Back
Top Bottom