NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
KOCHA msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', amefichua jambo akisema amezungumza na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' aliyeikaushia kambi ya Yanga akimtaka arejee klabuni hapo, ili kujihakikishia namba Stars kwani watamtathimini kabla ya kuitwa tena baadae
KOCHA msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', amefichua jambo akisema amezungumza na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' aliyeikaushia kambi ya Yanga akimtaka arejee klabuni hapo, ili kujihakikishia namba Stars kwani watamtathimini kabla ya kuitwa tena baadae.
Fei yupo nje ya Yanga tangu alipotangaza kuvunja mkataba na klabu hiyo na kuilipa Sh 112 Milioni zikiwamo za mishahara ya miezi mitatu, lakini klabu hiyo ikamgomea na kukimbilia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji inayomtambua ni mali ya timu hiyo.
Hata hivyo, licha ya kutokuwa na timu tangu Desemba makocha wa Stars walimuita na kumjumuisha kiungo huyo kwenye kikosi kilichocheza mechi mbili za kuwania tiketi za Afcon dhidi ya Uganda na ukizuka mjadala juu ya kiwango chake, lakini Morocco amevunja ukimya na kuzungumza mipango ya benchi la timu hiyo kwa mchezaji huyo kwa mechi zijazo baada ya kuzungumza naye.
Source mwanasport.
Nini maoni yako mdau wa mpira arejee yanga kula ugali na sukari au aendelee kukaa huko alipo ale vizuri ?