Kocha Morocco amrudisha Fei Toto Yanga

Kocha Morocco amrudisha Fei Toto Yanga

Yanga walivyo serious na maisha hana namba tena pale hakuna mtu wa kuwekwa bench na fei... Asubiri msimu uishe atafanyiwa uhuni hata sahau mpira wa bongo
Itakua kama kwa Morrison, msimu ukianza na jina lake linatangazwa ni mchezaji wa Yanga. Sasa sijui hapo yanga atafaidika nn maana anaendelea kumlipa na kazi hafanyi.
 
KOCHA msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', amefichua jambo akisema amezungumza na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' aliyeikaushia kambi ya Yanga akimtaka arejee klabuni hapo, ili kujihakikishia namba Stars kwani watamtathimini kabla ya kuitwa tena baadae

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa, Taifa Stars, Hemed Suleiman 'Morocco', amefichua jambo akisema amezungumza na kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' aliyeikaushia kambi ya Yanga akimtaka arejee klabuni hapo, ili kujihakikishia namba Stars kwani watamtathimini kabla ya kuitwa tena baadae.

Fei yupo nje ya Yanga tangu alipotangaza kuvunja mkataba na klabu hiyo na kuilipa Sh 112 Milioni zikiwamo za mishahara ya miezi mitatu, lakini klabu hiyo ikamgomea na kukimbilia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji inayomtambua ni mali ya timu hiyo.

Hata hivyo, licha ya kutokuwa na timu tangu Desemba makocha wa Stars walimuita na kumjumuisha kiungo huyo kwenye kikosi kilichocheza mechi mbili za kuwania tiketi za Afcon dhidi ya Uganda na ukizuka mjadala juu ya kiwango chake, lakini Morocco amevunja ukimya na kuzungumza mipango ya benchi la timu hiyo kwa mchezaji huyo kwa mechi zijazo baada ya kuzungumza naye.


Source mwanasport.

Nini maoni yako mdau wa mpira arejee yanga kula ugali na sukari au aendelee kukaa huko alipo ale vizuri ?
Yule mtoto wa baresa ni Simba lialia namkumbuka ,Simba ikifungwa wapambe wake wanapata tabu Sana
 
Kwamba FEI Toto hajawahi kuangalia ata behavior ya wachezaji wa Ulaya? Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu make timu inaweza kukuaribia kipaji chako wakati wowote.
Asitake huruma ya Yanga nje ya utaratibu wa mkataba...hii ndiyo sababu ya wenzetu waliweka utaratibu wa kuwa ba Agent. Kama aliashauriwa vibaya akatia wino kwenye mkataba inayomuumiza angevumilia hadi mwisho wakati huo anatafuta patakapomlipa vizuri.
 
Kwamba FEI Toto hajawahi kuangalia ata behavior ya wachezaji wa Ulaya? Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu make timu inaweza kukuaribia kipaji chako wakati wowote.
Asitake huruma ya Yanga nje ya utaratibu wa mkataba...hii ndiyo sababu ya wenzetu waliweka utaratibu wa kuwa ba Agent. Kama aliashauriwa vibaya akatia wino kwenye mkataba inayomuumiza angevumilia hadi mwisho wakati huo anatafuta patakapomlipa vizuri.
Kuna mapopoma yalimfuata yakachezea akili zake, akaona kabisa tayari yeye ni star kuliko timu
 
Back
Top Bottom