Kocha Mwinyi Zahera ameelemewa,asaidiwe ushauri nasaha

Mechi inayofuata, Zahera Anachaeza na Azam.
Nitafuatilia Kusikia Atakacho Zangumza Baada ya Mchezo.
Akifungwa tu Lazima Atailaumu Simba SC, na TFF.
Na Ndivyo Itakavyo Kuwa

Yanga SC kwa jinsi walivyoathirika Kisaikolojia kwa sasa nina wasiwasi kuwa huenda mechi yake na Azam FC basi Kipa Wao Kindoki akaingia Nyavuni mara Tano Kuokota mipira iliyoingia Golini Kwake. Tayari Yanga SC wameshavurugika na wanaanza kupotea kabisa. Naanza kuziona dalili za Watu Kuchapa Bakora pale Jangwani muda si mrefu.
 
Reactions: Tui
Huyu kocha alishazoea kuwina zile mechi za mwanzo ambazo nyingi alicheza nyumbani sana unapokwenda away kuna changamoto nyingi.

Na hapo bado. Watafungwa sana tu!
 
Reactions: BDN
sasa kuna maana gani ya ligi kama simba wanapendelewa? kama tff wanaipenda simba wazifute timu zote waibakize simba wawe wanawapa ubingwa kila mwaka bila kucheza. timu zote zinalalamika simba kubebwa unadhani ni wajinga?
 
yanga timu ya wananchi wazawa waafrika . simba timu ya wahindi na waarabu. wahindi wanawashangaa nyie waafrika kushabikia timu yao
 
sasa kuna maana gani ya ligi kama simba wanapendelewa? kama tff wanaipenda simba wazifute timu zote waibakize simba wawe wanawapa ubingwa kila mwaka bila kucheza. timu zote zinalalamika simba kubebwa unadhani ni wajinga?
Vp na kule kwenye azam federation simba wanabebwa, jana simba kacheza na coast na kaondoka baada ya game kurudi dar , hivi leo anaondoka kwenda kagera, kwa ratiba hii isiyo rafiki kwa afya za wachezaji bado unasema simba inabebwa
 
yanga timu ya wananchi wazawa waafrika . simba timu ya wahindi na waarabu. wahindi wanawashangaa nyie waafrika kushabikia timu yao
Kwani wahindi na waarabu sio watanzania, iyo Yanga ya Wazaramo mbona unaishangilia
 
Kwani wahindi na waarabu sio watanzania, iyo Yanga ya Wazaramo mbona unaishangilia
Mwache huyo mjamaa,
Huyo atakuwa ni yule alimuwemweka rehani mkewe siku Simba iliyomfunga Vita.
Ni aina ya washabiki wanaotaka timu yao ishinde kila mechi.
Ikiongozwa na kocha wao Zahera Mwinyimkuu.
Zahera hata hana tabia ya kuipongeza timu pinzani inayomfunga Yanga.
Yeye na washabiki wake wanaona ushindi ndio haki Ya Yanga Pekee
Na wanadai hiyo ni Timu ya Wananchi
Hivyo ni lazima wadekezwe na kupendelewa wao pekee.
Sisi wahamiaji tunaishangilia Simba isiyo na makuu.
 
Mkuu una hoja ya msingi lakini mengine sidhani kama uko sahihi. Ni kweli Zahera anapoteza muda Tanzania hilo halina ubishi. Pia malalamiko yake kuhusu mechi ya Jana ni sahihi kabisa hasa goli la Tambwe hata aliyelikataa ukimuuliza sasa hivi hawezi kueleza kwa nini alilikataa zaidi ya kusema "nilidhani". Lakini maamuzi hayo mabovu sidhani kama yanahusiana chochote na Simba. Kiujumla waamuzi wa Tanzania ni wa Ovyo kuliko hata neno lenyewe. Hawajui wanachokifanya na kwa ujumla baadhi ya waamuzi wanaochezesha ligi kuu walistahili kuchezesha ligi daraja la NNE.
 
Unaweza kuthibitisha maneno yako kama ni ya kweli?
Embu tuthibitishie maneno yako
kumbe historia ya simba na yanga huijui? yanga ilianzishwa mwaka 1935 na waafrika wazawa . simba ilianzishwa mwaka 1939 na wahindi na waarabu wa kariakoo, hawa wahindi na waarabu walikuwa hawaipendi yanga kwa sababu yanga ilikuwa timu ya waafrika, ndio wakaanzisha simba
 
Hii ndio Tz! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huyu kocha ana tabia za kiswahili swahili sana, ambapo kila janga linalompata mswahili husingizia watu wengine. Kauli kama nimerogwa, sipendwi, wananifitini, wananihujumu, ndio visingio vya haraka kuelezea magumu anayopitia mtu. Hata pale mtu ana ugonjwa uoelezeka na inajulikana unapatikana vipi, lakini bado watasingizia kurogwa na mawifi, majirani, n.k

Yanga, Simba, Coastal, Mtibwa zote zimepata short notice na zote zimecheza saa 8 mchana isipokuwa Zahara ndio anajifanya ana haki peke yake ya kutoa malalamiko ya kitotokitoto. Anadhani yeye ndio ana haki ya kutoa maoni peke yake ya malalamiko?

Uongozi wa Yanga uwe makini na kocha huyu, atawaingiza mkenge asipofungwa breki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…