Kocha Nabi ajiunga na Club ya Far Rabat ya Morroco

Mwache aende nao kwani mpira ni biashara sisi tunachotaka ni hela.
Mtapata kamisheni yenu ya udalali, pesa ya maana inaenda kwa mwenye mali.

Halafu timu zinazojielewa haziuzi wachezaji ambao bado wanawahitaji. Mnakubaliana na hali kishingo upande, si muda mrefu lawama kwa Hersi na GSM zitaanza. Watu niliowahi kuwataja kuwa Nabi ndiyo anaweza kuwachukua, nikasema Mayele si mmoja wao, ndiyo hao mpaka leo hawajaripoti kambini. Nadhani nina kitu....
 
Mtapata kamisheni yenu ya udalali, pesa ya maana inaenda kwa mwenye mali
Mtaumia sana ni mwendo wa Bil Bil na nyie kama mnahela njooni.

Kama ingekuwa hivyo Mayele angeuzwa bila Yanga kushirikishwa, Yanga ndiye alikuwa na final say kwenye issues ya Mayele. Tulikataa 115m tukapata 270m kwa Fei,hata huyo uwezo wa kukataa tulikuwa nao,sema ofa imetuvutia, so ww kama unazo zako ZILE 20B ambazo kila mkifungwa mnazikumbuka njoo nazo.
 
Unapata bil bil halafu unaenda kuokota yule beki wa Villa?
Ndio mpira ,yule wa Vila anaweza kuwa bora zaidi ya yule mule muokota Senegal,kwani Sawadogo mmemuokota wapi na Mudathir alipatikana wapi,then Sawadogo alifanya nini na Mudathir akafanya nini, bado kwa yule dogo mwengine Bacca wa tuliye muokota mapinduzi Zanzibar.

Mpira scouting ukiijua hutumii hela,nyingi mmewaokota wakina Okwa,Sawadogo, Quattara leo hii wote wana wadai.Wabongo mnapenda kusikia mchezaji katoka Senegal,Cameroon, Congo ndio muamini anajua. Hao wakina Kapombe,Shabalala walitoka wapi?.
 
Ubora labda aje kuupatia hapo puyanga. Na hao wachezaji walipatikana kwenye dirisha dogo lakini hauwezi kuniambia eti dirisha kubwa unauza wachezaji tegemeo kwa mabilioni kama mnavyodanganyana kwenye vijiwe vyenu halafu unaleta beki mwenye sifa za kujifunga. Uzeni wachezaji wenu wenyewe tuone kweli wana thamani na kama mnaamini katika falsafa hiyo ya kuuza wachezaji siyo mpaka mkasutwe Ikulu.

Timu maskini tu ndiyo zina mentality hiyo ya kudhani wachezaji wazuri ni wale wa bure au wa bei chee, Bayern wako tayari kumuuza Mane kwa hasara kubwa hana hata mwaka na wako mbioni kumreplace kwa Keane kwa gharama kubwa. Hayo ndiyo mambo timu zinazotambua zinafanya nini zinafanya.

Halafu jikite kwenye facts, nani kakuambia Outtara na Okwa wanaidai Simba?
 
Kwani tuliowauza wachezaji wa nani? Walikuwa na mkataba wa nani?Hivi Naymer ni mchezaji wa timu gani na nani ana maamuzi juu ya kuuzwa kwa Naymer?

Sasa wewe mwenyewe timu yako ina utajiri gani, mbona ulishindwa kumbakisha Konde Boy na Chama,unavizia mafree agent na wachezaji majeruhi.

Kuna hela sometimes huwezi kuzikataa Man Utd ni timu tajiri kuliko zote ulaya anabadilishana nafasi na Madrid still kamuuza CR7,ina maana nao hawakuwa na hela.


Okwa kuna intvw alifanya na CMG au Wasafi, alisema anawadai Kolo FC.
 
Haya Mayele akawatetemeshe manyonyo wanajeshi uko Marakech
Saa hii Inonga anatetema na Mayele huko kwenye timu yao ya taifa, sijui alijifunzia wapi..!!?? Au alipokuwa Tanzania, Inonga alikuwa anatetema chooni? Maana anapatia kishenzi..!!
 
Hiyo interview ya Okwa umeiona au kuisikia wewe peke yako maana hakuna kitu kama hicho. Outtara je? Na kwenye swali langu sijamtaja Sawadogo.

Na unasema mmeuza "wachezaji", kwani wachezaji gani mmewauza, nipe list. Miq na Chama kuuzwa ni kama ambavyo wengine tumekuwa tunasema kwa muda mrefu kuwa Sakho atakuja kuuzwa tena kwa pesa nyingi tukawa tunabezwa, leo ndiyo mnaelewa.
 
Haya kabishane na radio πŸ‘‡πŸ‘‡

Sakho huyu huyu, haya kauzwa kwa shilling ngapi Sakho...........?
 
Haya kabishane na radio πŸ‘‡πŸ‘‡
View attachment 2691976
Sakho huyu huyu, haya kauzwa kwa shilling ngapi Sakho...........?
Kumbe kacheleweshewa, mbona hilo linatokea kwa kila mtu unapofanya kazi na taasisi yoyote nchi hii. Yaani we kwa mtazamo wako unadhani Simba hii wanaweza kumdhurumu mchezaji wa kimataifa kwa kumuacha halafu wasimlipe stahiki zake bila kujua madhara yake? Na umemtaja Outtara, naye umesikia wapi?
 
Quattara nilisikia Wasafi nae anadai, halafu mbona mkiambiwa madeni ya Simba mnakuwa wakali,ila uzushi huu wa Yanga mnaukubali au ndie ile Nyani haoni lake Kund*le?

Kweli taasisi zina madeni na ndio maana Okwa,Sawadogo na Quattara wanawadai, hata Yanga nayo inadaiwa.
 
Hamna aliye mkali, najaribu tu kukuelewesha, tuweke ushabiki pembeni tuzungumze facts. Kwani mada ni madeni bwashee? Na hayo unayoita madeni unayokomalia, hata mwezi umefika kweli toka hao wachezaji wameachwa? Haya ni malipo yaliyo kwenye process ya kulipwa, unaongea utadhani ni madeni sugu. Tujikite kwenye hoja.
 
Unieleweshe nini sasa facts zangu zenye reference kutoka kwenye vyombo vya habari ulikuwa unazikataa. Sasa ww unaongea facts halafu huna reference watu si wanakuona mzushi.

Deni ni deni haijalishi lina siku ngapi.

Halafu hoja iliyo kuwepo ni hii ambayo ww umeidandia.
 
Rizki ya mtu haiwezi kuzuiwa na mwanadamu milele. Kuna watu walimpigia fitna kwa Kaizer, mchongo wake ukaungua sasa karudi kwa waarabu wenzake halafu mara paah Rabat wanapangwa na puyanga
Atawapiga kama ngoma
 
Unieleweshe nini sasa facts zangu zenye reference kutoka kwenye vyombo vya habari ulikuwa unazikataa. Sasa ww unaongea facts halafu huna reference watu si wanakuona mzushi.

Deni ni deni haijalishi lina siku ngapi.
Umesema umesikia Wasafi wamesema, kwa hiyo nikuamini tu kwa kauli hiyo? Na Wasafi ipi unayotokea kuiamini sana, hii yenye kipindi kilichojikita kwenye tetesi? Na kwa kuwa unasema una ufahamu sana kwenye masuala ya malipo ya wachezaji, kawaida inachukua muda gani malipo tena ya mchezaji wa kimataifa kufanyika? Kumbuka hata dirisha la usajili halijafungwa. Tafuta mengine ya kuwasema Simba, kwenye hili unapuyanga tu.
 
Kwa nini Yanga tumemuacha manywele aondoke kirahisi
 
Kwani zile za Sawadogo na Okwa si nimekuletea reference mbona ulikiwa mgumu kuto kuamini.

Hivi una elewa funga na fungua semi kwenye uandishi wa habari zina maanisha nini au husomagi magazeti? Wasafi wameripoti alicho kilipoti mchezaji na ndio maana unaona funga na fungua semi, hamna tetesi bali ni habari kamili kutoka kwenye source yenyewe ambayo ni mchezaji amesema.

Nimeanza kuwasemea Simba lini wakati wachezaji wao ndio waliosema.Swala sijui kuchukua mda gani si fahamu ila ninacho fahamu Okwa,Sawadogo na Quattara wanawadai Simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…