SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wakati maumivu ya kuondoka kwa "Profesa" Nabi bado hayajapoa, kumekuwa na uvumi kuwa kuna uwezekano baadhi ya wachezaji akiwemo Fiston Mayele kujiunga naye huko alipokwenda.
Ukweli ni kuwa Mayele pamoja na Aziz Ki ni baadhi ya wachezaji aliokuwa anawavumilia tu kutokana na kuwa ni vipenzi vya mashabiki na viongozi. Ila ukweli ni kuwa mapungufu hasa ya Aziz Ki yalikuwa yanamuumiza kichwa sana hadi kupelekea mara kadhaa kumuweka benchi au kumtoa hata kama ametoka kufunga goli.
Kwa upande wa Mayele, ni mchezaji anayejituma sana na alimpenda kwa hilo ila upungufu wake mkubwa ni kuwa mzito kushea mipira kwa wenzake walio kwenye nafasi nzuri zaidi za kufunga na pia siyo mtumiaji mzuri sana wa nafasi. Mayele ni ngumu sana kuvutia timu yoyote kubwa kutokana na sababu hizi.
Wachezaji ambao walikuwa vipenzi vya Nabi ambao hadi wakati anaondoka walikuwa na viwango vya kuridhisha ni Diarra, Bacca, Dickson Job na Aucho. Kama mnadhani kuna mchezaji anaweza kumchukua waangalieni hao.