Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 24,606
- 39,289
Mabingwa wa Kihistoria, Timu ya Wananchi, Vijana wa Jangwani na Vinara wa Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young African Sports Club wanadaiwa kumpa mikoba Kocha, Nasreddine Nabi iliyoachwa na mtangulizi wake Cedric Kaze.
Nasreddine Nabi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya El Merreikh atachukua nafasi hiyo ambayo kwa sasa inakaimiwa na Juma Mwambusi.
Kwa mujibu wa tetesi zilizopo ni kuwa Kocha huyo Mpya wa yanga anatarajiwa Kuwasili rasmi Nchini hapo kesho siku ya Jumanne akiwa na benchi lake la ufundi.
Kocha huyo raia wa Tunisia ni muumini wa mfumo wa 4-1-4-1 na anauzoefu na soka la Afrika.